Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 22:06

Watu 13 wauawa katika mapigano nje ya mji mkuu Bujumbura


Mfanyakazi wa Burundi kutoka katika Kamisheni ya Ukweli na Suluhu akitoa fuvu la mtu aliyekuwa hajatambulikana kutoka katika kaburi la watu waliozikwa pamoja nchini humo. REUTERS/Evrard Ngendakumana - RC21PE9DJA9D
Mfanyakazi wa Burundi kutoka katika Kamisheni ya Ukweli na Suluhu akitoa fuvu la mtu aliyekuwa hajatambulikana kutoka katika kaburi la watu waliozikwa pamoja nchini humo. REUTERS/Evrard Ngendakumana - RC21PE9DJA9D

Watu 12 wenye silaha wameripotiwa kuuawa katika mapigano na vikosi vya kulinda usalama vya serikali ya Burundi, yaliotokea jumapili katika wilaya mojakusini mwa mji mkuu Bujumbura.

Kiongozi wa wilaya ya Nyabiraba, Ferdinand Simbananiye amewaambia waandishi wa habari kwamba kundi lenye wapiganaji 14 lisilojulikana lilishambulia wilaya yake Jumapili, 12 miongoni mwao waliuawa, katika makabiliano na jeshi la polisi.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa askari polisi moja pia aliuawa katika mapigano hayo, huku wapiganaji 2 wakikamatwa na silaha zao 6 kupokonywa.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo.

Taarifa zinasema wakazi wa wilaya hiyo iliyopo mkoa wa Bujumbura vijijini, hasa wafuasi wa chama cha upinzani cha CNL wana wasiwasi mkubwa baada ya kutokea mapigano hayo.

Wafuasi wa chama cha CNL cha naibu spika wa bunge Agathon Rwasa, wamekuwa wakilalamika kwamba wanakamatwa kiholela na polisi, ikiwashutumu kuhusika katika harakati za kuvuruga usalama.

Chama hicho kimepinga mara kadha tuhuma hizo za polisi, na kudai kwamba wafwasi wake wananyanyaswa kwa sababu ya misingi ya kisiasa.

Burundi ambayo inakumbwa na mzozo wa kisiasa tangu April 2015, inajianda kuelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Mei 2020. Rais aliyeko madarakani, Pierre Nkurunziza hatagombea tena baada ya kuhudumu mihula mitatu tangu mwaka wa 2005.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG