Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Agosti 02, 2021 Local time: 21:18

Mamia wajitokeza kumzika Kizito Mihigo, Rwanda yatakiwa kuruhusu uchunguzi huru


Kizito Mihigo

Mamia ya wananchi wa Rwanda wamejitokeza Jumamosi kuuaga mwili wa msanii maarufu wa nyimbo za Injili Kizito Mihigo, akiwemo Diane Rwigara, mwanasiasa wa upinzani na mfanyabiashara mjini Kigali.

Kifo cha Mihigo kimeibua hisia mseto kati ya wananchi wa Rwanda wanaoishi ndani na nje ya nchi.

Pia kumekuwa na shinikizo kwa serikali ya Rwanda kuruhusu uchunguzi huru ufanyike ili ipate kujulikana kilicho sababisha kifo chake.

Mashirika ya kibinadamu pia yalitilia shaka kifo chake na kutaka uchunguzi huru ufanyike kuhusiana na kifo hicho.

Hata hivyo Rwanda imepinga shinikizo kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu ya kutaka uchunguzi huru kufanywa kuhusu kifo cha msanii maarufu wa muziki wa kiinjili Kizito Mihigo.

Mihigo ambaye aliripotiwa kujiua katika mahabusu ya polisi nchini Rwanda anazikwa leo nchini Rwanda. Maombi kwa ajili ya Kizito yamefanyika katika Kanisa Katoliki la Indera mjini Kigali, Rwanda.

Marehemu alifariki siku tatu baada ya kukamatwa karibu na mpaka wa Burundi, polisi wakimtuhumu kuwa alitaka kutoroka nchini na kujiunga na kundi la waasi lenye kufanya harakati dhidi ya serikali ya Rwanda.

Vyanzo vya habari nchini Rwanda vimesema Mihigo alipigwa marufuku kuondoka nchini Rwanda kutokana na kukabiliwa na mashitaka yaliyofunguliwa na serikali ya Rwanda dhidi yake.

Kizito mihigo alikua ni mtunzi na muimbaji maarufu wa nyimbo za injili zilizo wafurahisha na kuwaburudisha Wanyarwanda na Warundi ndani na nje ya nchi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG