Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 26, 2022 Local time: 15:58

Watano wafariki, darzeni hawajulikani walipo ajali ya feri Bangladesh


Watu wakusanyika pembeni ya mto Shitalakshya, ambako feri ya kubeba abiria imezama baada ya kugongana na meli ya mizigo mjini Narayanganj (Picha na Reuters)

Watu watano wameuawa na wengine kadhaa hawajulikani walipo, baada ya meli ya kubeba mizigo kuigonga feri ya abiria nchini Bangladesh.

Polisi wamesema kwamba karibu darzeni mbili ya watu wamefanikiwa kuogelea na kunusurika kifo baada ya meli ya mizigo MV Afsaruddin, kuigonga feri MV Ruposhi -9 kusini mashariki mwa Dhaka.

Video inayoonyesha feri hiyo ikizama ina watu wanaopiga mayowe kuomba kuokolewa.

Mkuu wa polisi Aslam Mia, amesema kwamba feri hiyo ilikuwa imebeba zaidi ya abiria 60.

Abiria 22 kati yao walifanikiwa kuogelea na kujiokoa.

Mkuu wa wilaya Monjurul Hafiz, amesema kuwa walinzi wa pwani na watu wenye ujuezi wa kuogelea wanasaidia katika kuwatafuta waathirika.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG