Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 11:29

Feri yawaka moto Bangladesh, 39 wauawa


Watu wakipanda Feri, Munshiganj, Bangladesh. [Maktaba]
Watu wakipanda Feri, Munshiganj, Bangladesh. [Maktaba]

Moto mkubwa umetokea ndani ya feri iliyojaa watu kupita kiasi kusini mwa Bangladesh na kusababisha vifo vya watu 39 na wengine 72 kujeruhiwa.

Abiria walionekana wakiruka kutoka kwenye feri hiyo na kuogelea.

Maafisa wamesema kwamba moto huo umeanzia kwenye chumba chenye injini ya feri.

Afisa wa polisi Syed Mahabubur Rahman, amesema kwamba injini iliendelea kufanya kazi kwa muda wa saa nzima huku ikiwaka moto.

Feri hiyo imevutwa hadi kwenye ufukweni baada ya moto kuzimwa.

Feri hiyo ilikuwa inatoka mji mkuu wa Dhaka hadi Barguma, umbali wa kilomita 250.

Waokoaji wamepata miili ya watu 39 na watu 72 waliojeruhiwa wamelazwa hospitalini ikiwemo saba ambao wameungua vibaya, na ambao hali yao ni mbaya.

Serikali imeunda kamati mbili kuchunguza kilichosababisha moto huo. Kamati hizo zina mda wa siku tatu kuasilisha ripoti.

XS
SM
MD
LG