Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 17:43

Wasudan wanadai kuwa na imani na mazungumzo ya Jeddah


Moshi ukifuka angani huko kusini mwa jiji la Khartoum wakati mapigano yakiendelea tarehe 6, Mei 2023. Picha na AFP.
Moshi ukifuka angani huko kusini mwa jiji la Khartoum wakati mapigano yakiendelea tarehe 6, Mei 2023. Picha na AFP.

Raia nchini Sudan wana matumaini mazungumzo kati ya wajumbe wa pande zinazopigana yanayofanyika huko Jeddah nchini Saudi Arabia kusitisha umwagaji damu ambao umesababisha mamia ya watu kupoteza maisha na wengi kuyakimbia makazi yao.

Lakini hakuna dalili kwa afueni ya kudumu katika siku za hivi karibuni.

Hakuna tamko lolote kuhusiana na maendeleo ya mazungumzo hayo ambayo yalianza siku ya Jumamosi kati ya jeshi na kikosi hasimu kinachojulikana kama Rapid Support Forces (RSF) yanayofanyika katika mji wa bandari ulioko katika bahari ya Shamu nchini Saudi Arabia.

Pande hizo zinazopigana zimesema zitajaribu kushughulikia upitishaji salama wa mahitaji ya kibinadamu na siyo kumaliza wa vita. Makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano yamekiukwa tangu mzozo ulipozuka Aprili 15.

"Iwapo mashauriano ya Jeddah yatashindwa kusitisha vita, hii itaimanisha kuwa hatutaweza kurejea majumbani mwetu na kwenye maisha yetu," alisema Tamader Ibrahim, mtumishi wa serikali mwenye umri wa miaka 35 aliyeko katika mji wa Bahri, ng'ambo ya mto wa Blue Nile kutoka Khartoum

"Tunasubiri mashauriano haya kwa sababu ndiyo matumaini yetu pekee." Mahjoub Salah, daktari mwenye umri wa miaka 28, alisema maeneo ya mji mkuu yaliyokumbwa na ghasia hubadilika siku hadi siku.

Salah alishuhudia mapigano makali wakati jirani yake alipopigwa risasi tumboni alipokuwa katika eneo lake la wilaya Al Amarat iliyopo katikati ya mji wa Khartoum mwezi uliopita, kabla ya kukodi nyumba kwa ajili ya familia yake kusini-mashariki mwa mji mkuu.

"Bado tunasubiri hati zetu za kusafiria zitoke, lakini hatujui hii itachukua muda gani," Salah alisema. "Kisha mpango wetu ni kusafiri kutoka Port Sudan kwenda Saudi Arabia."

Juhudi za Marekani na Saudi Arabia ni jaribio la kwanza kubwa la kusitisha mapigano ambayo yamezigeuza baadhi ya sehemu za Khartoum kuwa uwanjwa wa mapigano, na kuvuruga mpango unaoungwa mkono kimataifa uliolenga kuleta utawala wa raia baada ya miaka mingi ya machafuko, na kusababisha migogoro ya kibinadamu.

Baadhi ya taarifa ya habari hii inatoka Shirika la habari la

XS
SM
MD
LG