Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 06, 2023 Local time: 18:29

Ndege za kivita za Sudan zaendelea kufanya mashambulizi ya angani Khartoum


Moshi ukitanda Khartoum katikati ya mapigano kati ya vikosi vya majenerali mahasimu wa Sudan Mei 6, 2023.

Ndege za kivita za Sudan zimeendelea kufanya  mashambulizi ya anga katika mji mkuu wa Khartoum na miji mingine iliyo karibu ya Bahri na Omdurman licha ya kuwepo mazungumzo ya sitisho la mapigano yanayoendelea Saudi  Arabia.

Mashambulizi ya ardhini yanaendelea baina ya jeshi na kikosi cha RSF katika maeneo mawili katikati mwa Bahri –Shambat na Halfiya.

Mapigano huko Shambat yalifanyika karibu na kambi kubwa ya jeshi wakati mapigano Halfiya yanaonekana ni kutaka kudhibiti daraja kubwa ambalo sasa liko kwenye udhibiti wa RSF. Mapigano yametaabisha watu na kuwalazimisha kujificha katika nyumba zao.

Mapigano makali baina ya jeshi na wanamgambo wa RSF, ambayo yamekuwa yakiendelea kwa wiki tatu sasa, yameua mamia ya watu na kusukuma taifa hilo la Afrika kuelekea kuanguka.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya Saudi Arabia na Marekani , mashauriano ya kwanza kabisa tangu mzozo wa kugombea madaraka ulipozuka April 15 yanafanyika katika mji wa mwambao wa Jeddah , Saudi Arabia, katika bahari ya Sham.

Mazungumzo hayo ni sehemu ya juhudi za kidiplomasia zilizopendekezwa na Saudi Arabia na Marekani kwa lengo la kusitisha mapigano ambayo yameibadilisha Khartoum na maeneo mengine mijini kuwa sehemu ya mapambano ambayo yamesababisha maelfu ya watu kutoroka nyumba zao.

XS
SM
MD
LG