Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 05:16

Washukiwa 13 wa dawa za kulevya wakamatwa Kenya


Kushoto Baktash Akasha, Gulam Hussein, Ibrahim Akasha na Vijaygiri Goswami
Kushoto Baktash Akasha, Gulam Hussein, Ibrahim Akasha na Vijaygiri Goswami

Vyombo vya usalama Kenya vimewakamata washukiwa 13 wa ulanguzi wa dawa za kulevya mjini Mombasa, Alhamisi usiku.

Kamanda wa Polisi eneo la Pwani Philip Tuimur amewaambia waandishi wa habari kuwa, waliokamatwa ni pamoja na raia 3 wa Italy, raia mmoja wa Mauritius, Mtanzania mmoja na Wakenya 8 wakiwapo wanawake wawili.

Kwa mujibu wa taarifa hizo washukiwa hao ni sehemu ya mtandao wa kimataifa unaohusika na usambazai wa dawa za kulevya katika nchi za Kenya, Tanzania, Ushelisheli, Mauritius na nchi zingine.

Kamanda Tumur amesema wanajiandaa kuwafungulia mashtaka washukiwa hao, na hatua nyingine itakuwa kuwarejesha makwao Waitaliano hao watatu.

Mtanzania aliyekamatwa ametajwa na polisi kuwa mtu aliyehusika na visa kadhaa vya wizi wa mabavu nchini Kenya, na amewahi kutumikia kufungo katika magereza ya Mombasa.

Naye raia wa Mauritius anaeshikiliwa na polisi amekuwa akifanya kazi kama promota wa muziki eneo la pwani kwa kuwasajili wasanii chipukizi, na sasa anahusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya.

Msako dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya umechacha Mombasa na pwani ya Kenya kwa jumla tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Washukiwa wengine wakuu kutoka familia ya marehemu Akasha walishtakiwa pamoja na raia wengine wa kigeni, na baadaye kusafirishwa Januari kujibu mashtaka katika mahakama moja ya New York, Marekani.

XS
SM
MD
LG