Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 07:19

Washirika wa Somalia wapongeza kuchaguliwa Rais Mohamud


Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud
Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud

Washirika wa kimataifa wa Somalia Jumatatu wamepongeza kuchaguliwa kwa Hassan Sheikh Mohamud rais ajaye wa taifa hilo.

Mohamud anachukua madaraka baada ya miezi kadhaa ya ukosefu wa uthabiti wa kisiasa, huku nchi hiyo ikikabiliwa na uasi wenye ghasia na ukame mbaya.

Wakaazi katika mji mkuu, Mogadishu waliingia mitaani wakiimba na kugonga makopo na kufyatua fataki hewani kusherehekea matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa majira ya saa sita usiku.

Wengi wanatarajia kwamba upigaji kura uliomalizika kwa amani lakini uligubikwa na madai ya dosari utamaliza mzozo wa kisiasa ambao umedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Rais wa Somalia anayeondoka madarakani Mohamed Abdullahi Mohamed muhula wake ulikamilika mwezi February mwaka 2021, bila kuwepo uchaguzi na mzozo wa muda mrefu wa kugombea madaraka uliofuata, uligeuka kuwa vurugu wakati fulani na kusababisha migawanyiko katika ngazi za juu serikalini.

XS
SM
MD
LG