Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 20:41

Wapiganaji wa Tigray wakubali kushiriki mchakato wa amani unaosimamiwa na AU


Wapiganaji wa Tigray
Wapiganaji wa Tigray

Wanamgambo wa Tigray nchini Ethiopia walisema Jumapili wako tayari kwa usitishaji mapigano na watakubali mchakato wa amani unaoongozwa na Umoja wa Afrika, kuondoa kikwazo katika mazungumzo na serikali ili kumaliza karibu miaka miwili ya vita vya kikatili.

Tangazo hilo lilitolewa huku kukiwa na juhudi mbalimbali za diplomasia ya kimataifa baada ya mapigano kupamba moto mwezi uliopita kwa mara ya kwanza katika miezi kadhaa kaskazini mwa Ethiopia.

"Serikali ya Tigray iko tayari kushiriki katika mchakato thabiti wa amani chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika," ilisema taarifa ya mamlaka ya Tigray.

"Zaidi ya hayo, tuko tayari kutii usitishaji wa mara moja na uliokubaliwa kwa pande zote mbili wa uhasama ili kuweka mazingira mazuri," iliongeza.

Serikali ya Ethiopia hapo awali ilisema iko tayari kwa mazungumzo yasiyo na masharti "wakati wowote, mahali popote," yaliyosimamiwa na AU yenye makao yake makuu mjini Addis Ababa.

Chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) hadi sasa kilikuwa kimepinga vikali jukumu la mjumbe wa AU katika Pembe ya Afrika Olusegun Obasanjo, kikilalamikia "ukaribu" wake na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.

Mkuu wa Tume ya AU Moussa Faki Mahamat alitoa taarifa ya kukaribisha hatua hiyo kama "fursa ya kipekee kuelekea kurejesha amani" na kuzitaka "pande zote mbili kufanya kazi kwa haraka kuelekea usitishaji mapigano mara moja, na kushiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja".

XS
SM
MD
LG