Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 27, 2022 Local time: 01:57

Mapigano yazuka kati ya vikosi vya Tigray na serikali kuu Ethiopia


Wanajeshi wa serikali ya Ethiopia kwenye barabara karibu na Agula, kaskazini mwa Mekele, katika eneo la Tigray. (AP Photo/Ben Curtis)

Mapigano kati ya vikosi vya eneo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray na vikosi vya serikali kuu yamezuka karibu na mji wa Kobo, wakaazi na pande zote mbili walisema leo Jumatano, na kumaliza usitishaji wa mapigano uliodumu kwa miezi kadhaa.

Mapigano hayo ni pigo kubwa kwa matumaini ya mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed na chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF), chama kinachodhibiti Tigray.

Pande zote mbili zimelaumiana kwa kuzuka kwa mapigano.

Saa tano asubuhi leo (TPLF) wameshambulia upande wa Mashariki, kutoka Bisober, Zobel na Tekulshe, kwa kufanyahivyo wamevunja rasmi usitishaji wa mapigano, idara ya mawasiliano ya serikali ilisema katika taarifa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG