Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:30

Kenya yachagua viongozi wake kitaifa


Wananchi wakiwa tayari kupiga kura katika eneo la Gatundu, kaunti ya Kiambu, Kenya, Aug. 8, 2017.
Wananchi wakiwa tayari kupiga kura katika eneo la Gatundu, kaunti ya Kiambu, Kenya, Aug. 8, 2017.

Raia wa Kenya asubuhi hii wanaelekea katika vituo vya kupigia kura kushiriki kuwachagua viongozi wao.

Uchaguzi huu ni mmoja wa uchaguzi unaoangaliwa kwa ukaribu barani Afrika, ambapo rais aliye madarakani sasa Uhuru Kenyatta anagombania wadhifa huo akikabiliana na mpinzani wake wa siku nyingi, kiongozi wa upinzani Raila Odinga katika kiti cha urais.

Mchuano katika uchaguzi huu wa leo unaelezwa kuwa mkubwa. Rais Uhuru Kenyatta ametoa mwito kwa wapiga kura wa nchini humo kupiga kura kwa amani.

Kenyatta na Odinga waligombania urais katika uchaguzi wa mwaka 2013 na raia wengi wa Kenya wanasema kampeni za wanasiasa hao hazijawahi kumalizika.

XS
SM
MD
LG