Wanahabari wa VOA waliopo nchini humo wameshuhudia raia wa Kenya, wakipanga mistari majira ya saa kumi usiku ikiwa ni mapema zaidi kabla ya muda uliopangwa wa vituo vya kura kufunguliwa.
Kenya inaingia katika uchaguzi mkuu asubuhi majira ya Afrika Mashariki, uchaguzi ambao unatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa baina ya rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee, na Raila Odinga wa muungano wa NASA.
VOA itakupasha kila kinachoendelea nchini humo mpaka matokeo yatakapotangazwa na kuapishwa kwa rais na matukio yote yanayohusiana na uchaguzi huo.
Mistari ya wapiga kura ilionekana mapema alfajiri ya leo tarehe 8 mwezi Agosti, mwaka 2017, ambayo ni siku ya upigaji kura nchini Kenya kwa ajili ya uchaguzi mkuu.