Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 11:53

Wanachama wa WHO wakubaliana kuboresha huduma za afya


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus akihutubia mkutano wa 72 wa afya duniani, Geneva, Uswizi, Mei 20, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus akihutubia mkutano wa 72 wa afya duniani, Geneva, Uswizi, Mei 20, 2019.

Mkutano wa 72 wa afya duniani umemalizika mjini Geneva, Uswizi, wanachama wa Shirika la Afya Duniani,WHO, wakifikia makubaliano ya kuboresha huduma za afya ya msingi kote ulimwenguni.

Kauli mbiu ya mwaka 2019 inaujumbe unaosema “Huduma ya afya kwa wote, hakuna atakaye achwa nyuma.”

Mkutano huo wa siku tisa umetoa wito wa kupatikana mpango wa kimataifa kuboresha huduma za msingi katika kila nchi.

Mkurugenzi Mkuu wa – WHO – Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema wote wanawajibu wa kuwekeza kwa kiwango cha hali ya juu katika huduma za msingi za afya, kutekeleza muongozo wa - WHO – kwa wafanyakazi wa afya, na kuhakikisha kuna mazingira bora kwa upatikanaji wa huduma za afya kwa wote.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG