Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 16:30

Siku ya Saratani Duniani 2019: Ijue saratani ya shingo ya kizazi


Siku ya saratani duniani
Siku ya saratani duniani

Shirika la Afya Duniani (WHO) linataka hatua ziharakishwe zaidi katika kupunguza saratani ya shingo ya kizazi, ugonjwa ambao unaweza kuzuilika lakini unaua zaidi ya wanawake 300,000 kila mwaka, wengi wao kutoka nchi zinazoendelea.

Wakati dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya saratani Jumatatu Februari 4, saratani ya shingo ya kizazi ni moja ya sababu kuu za vifo kwa wanawake duniani kote.

Vifo tisa kati ya 10 vinatokea katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati. Ugonjwa huu unasababishwa na kirusi kinachojulikana kama ‘Human Pappiloma Virus’ na huambukizwa kwa njia ya mapenzi.

Tiba ya saratani hiyo

WHO inasema saratani ya shingo ya kizazi inaweza kutibiwa kama maambukizi yatagunduliwa mapema na kutibiwa katika hatua za awali. Lakini, kama ilivyo kwa magonjwa mengine katika maisha, kuzuia ndiyo njia bora zaidi. Kuhusu saratani ya shingo ya kizazi, chanjo inayofanya kazi vizuri inapatikana na inaweza kuzuia ugonjwa huu pale wasichana walio na umri kati ya mitaka tisa na 14 watapatiwa chanjo ya kuzuia.

Afisa ambaye anashughulika na masuala ya chanjo katika WHO, Paul Bloem anasema chanjo kwa kiasi kikubwa inatolewa katika nchi tajiri. Wakati nchi zenye mzigo mkubwa wa saratani ya shingo ya kizazi barani Afrika na Asia yako nyuma sana, anasema lakini maendeleo kiasi yametokea.

Kuzinduliwa kwa chanjo

“Nchi kama vile Rwanda, ambayo ni kiongozi barani Afrika imeweza kuwafikia zaidi ya asilimia 90 katika kipindi cha miaka mitano au sita. Bhutan pia inawafikia asilimia 90 ya wasichana. Malaysia imewafikia asilimia 97 ya wasichana wake. Kwahiyo, kuna mifano mizuri mizuri sana ambayo inaonyesha kwamba chanjo hii inakubalika na inakubalika na inaweza kutolewa hata kwenye nchi zenye kipato cha chini,” amesema Bloem.

Boem anasema nchi nne za Afrika nazo ni Tanzania, Ethiopia, Zimbabwe na Senegal, ambayo ilizinduliwa mwaka jana. Anasema nchi 11 zaidi za Afrika na Asia zitaanza kuitumia chanjo hii baadaye mwaka huu.

Ukosefu wa wataalam

Princess Nothemba Simelela ambaye ni mkurugenzi mkuu msaidiziwa WHO katika masuala ya familia, wanawake na watoto. Anasema tatizo kubwa ni nchi zinazoendelea zina ukosefu wa watu wenye ujuzi kuwapima wanawake na kuwatambua kama wana saratani ya shingo ya kizazi.

Anasema kwamba wanawake katika maeneo ya ndani sana ya vijijini, mara nyingi inakuwa vigumu kufika kwenye kliniki ambako wanaweza kupimwana kutibiwa. Lakini ameiambia VOA kuna mikakati ya serikali ambayo inaweza kulishughulikia suala hili na kupata matokeo chanya.

“Tunaweza kuwa na kliniki zinazohamishika. Mara nyingine, ulichonacho ni siku ambapo wanawake wanaweza kuitwa au wasichana wadogo wanaweza kufika kwenye hizo kliniki ili kuangaliwa kiafya,” Simelela anasema.

Anasema mkakati mwingine ni kwamba serikali zinaweza kutumia program za shule za fya. Kwa mfano, anasema Rwanda na Afrika Kusini wamefikisha chanjo katika shule ambako inatolewa kwa idadi kubwa ya wasichana katika umri ambao unaelezewa ni muhimu kupatiwa chanjo hii.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Khadija Riyami, Washington, DC

XS
SM
MD
LG