Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 03, 2022 Local time: 11:12

Waliouawa katika kituo cha kulea watoto Thailand ni zaidi ya watu 30


Watu waliopoteza ndugu zao wakijifariji katika kituo cha kulea watoto Thailand ambapo mtu mwenye silaha anadaiwa kuwauwa zaidi ya watu 30.

Polisi nchini Thailand wanasema mtu mwenye bunduki amekishambulia kituo cha kulea watoto katika mji wa kaskazini mashariki wa Nongbua Lamphu siku ya Alhamisi, na kuua zaidi ya watu 30.

Kati ya waliofariki ni watoto 23.

Kituo cha kulea watoto ambapo shambulizi la bunduki lilitokea Thailand.
Kituo cha kulea watoto ambapo shambulizi la bunduki lilitokea Thailand.

Mamlaka zilisema mshambuliaji huyo alirejea nyumbani na kumuua mke wake na mtoto kabla ya kujiua yeye mwenyewe.

Wamemtambua mtu huyo aliyekuwa na bunduki, ambaye pia alibeba kisu, kama ni afisa wa zamani wa polisi ambaye aliachishwa kazi katika jeshi la polisi mwaka 2021 kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.

Mauaji ya watu wengi ni nadra kutokea Thailand.

Baadhi ya taarifa katika repoti hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG