Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 11:58

Magavana Marekani waunda kikosi kazi kushughulikia mauaji mashuleni


Reggie Daniels akiomboleza katika Shule ya Msingi ya Robb, June 9, 2022, huko Uvalde, Texas.
Reggie Daniels akiomboleza katika Shule ya Msingi ya Robb, June 9, 2022, huko Uvalde, Texas.

Viongozi wa Chama cha  Kitaifa cha Magavana  Marekani wamesema Ijumaa wanaunda kikundi kazi kutoka vyama vyote vya siasa nchini humo ili kutoa mapendekezo ya kuzuia mauaji ya halaiki kufuatia yale yaliyofanyika katika shule moja huko  Texas.

Kufikia makubaliano huenda lisiwe jambo rahisi kwa vile magavana wa Marekani wamegawanyika katika misingi ya vyama vyao kushughulikia masuala ya udhibiti wa bunduki na usalama mashuleni.

Gavana wa Mrepublikan Asa Hutchinson wa Arkansas, mwenyekiti wa kikundi hicho, na Gavana Mdemokrat Phil Murphy wa New Jersey, makamu mwenyekiti, wameiambia White House katika barua waliyotuma kuwa watakutana kikundi cha magavana sita hadi kumi, na kuangazia hasa kuhakikisha usalama mashuleni.

Hutchinson na Murphy walionekana kuacha wazi uwezekano wa mapendekezo hayo kujumuisha baadhi ya ushauri wa aina za udhibiti wa bunduki. Baraza la Wawakilishi la Marekani wiki hii liliidhinisha mswaada wa hatua pana kadhaa za udhibiti wa bunduki ambao una nafasi ndogo sana kupitishwa na Baraza la Seneti.

Barua hiyo imetolewa wakati magavana wamegawanyika kwa mrengo wa vyama vyao juu ya njia bora ya kukabiliana na mauaji ya wanafunzi 19 wa shule ya msingi huko Uvalde, Texas na walimu wao wawili. Ukusanyaji maoni wa karibuni uliofanywa na shirika la habari la AP umeonyesha magavana wamegawanyika, huku Wademokrat wakitaka kuwepo masharti zaidi ya udhibiti wa bunduki na Warepublikan wakilenga badala yake katika kuimarisha ulinzi mashuleni.

Hutchinson amesema kuwa kuongeza kiwango cha umri kwa ununuzi wa bunduki aina ya AR uwe kutoka miaka 18 hadi 21 iwe ni sehemu ya majadiliano. Lakini Hutchinson, ambaye anaachia madaraka mwezi Januari na anafikiria kugombea nafasi ya urais, hajazungumzia kuwepo kwa hatua kama hiyo katika jimbo lake na amesema hatua za udhibiti wa bunduki hazitakuwa katika ajenda iwapo atalitaka Baraza la Wawakilishi la jimbo hilo linalodhibitiwa na Warepublikan kufuata ushauri wa usalama mashuleni katika kikao maalum kinachoweza kufanyika.

Barua hiyo ilitumwa siku hiyo hiyo Hutchinson alipotangaza kuwa anarejesha kamati ya usalama mashuleni aliyoiunda ili ije na mapendekezo kufuatia mauaji katika shule moja mwaka 2018 huko Parkland, Florida.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Associated Press

XS
SM
MD
LG