Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 02:51

Biden ametaka wabunge kuweka sheria kali kuhusu ununuzi wa bunduki


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden amelitaka bunge kuchukua hatua na kukabiliana na mashambulizi ya risasi ambayo amesema yamegeuza shule, maduka ya jumla na sehemu nyingine ambazo huwa na watu wengi kila siku, kuwa uwanja wa mauaji.

Biden amesema kwamba yametosha, na kuonya kama wabunge watashindwa kuchukua hatua, wapiga kura wanastahili kuonyesha hasira zao kupitia upigaji kura wakati wa uchaguzi wa kati kati ya m uhula, utakaofanyika mwezi Novemba.

Biden alikuwa akizungumza kutoka white house, alhamisi jioni, ambapo alikiri kuwepo upinzani wa kisiasa kuhusiana na namna ya kudhibithi mashambulizi ya risasi yanayotekelezwa na raia na ambayo yamesababisha vifo vya watu kadhaa nchini Marekani.

Biden ametaka marufuku kuwekwa kwa uuzaji wa bunduki zinazofyatua risasi nyingi kwa wakati mmoja, na kusema kwamba iwapo bunge halitakubaliana na mapendekezo yake yote, basi ni lazima wabunge wahakikishe kwamba watu wenye matatizo ya akili hawaruhusiwi kumiliki bunduki, sawa na kuongeza umri kwa wanaonunua bunduki zenye uwezo wa kufyatua risasi nyingi kwa wakati mmoja, kutoka miaka 18 hadi 21.

XS
SM
MD
LG