Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 16:27

Shambulizi lililosababisha vifo vya watu 6 Illinois lafufua mjadala wa umiliki bunduki Marekani


Eneo la mashambulizi ya Julai 4, 2022
Eneo la mashambulizi ya Julai 4, 2022

Risala za rambirambi zimeendelea kutolewa, kwa familia za watu waliopoteza maisha yao jana Jumatatu, baada ya mtu mwenye silaha akiwa juu ya paa, kufyatua risasi kwenye gwaride la kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Marekani.

Shambulzi hilo lilifanyika katika kitongoji kimoja mjini Chicago, jimbo la Illinois, na kuua takriban watu sita, na kujeruhi takriban 30.

Mamlaka zilisema mtu mmoja aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi Jumatatu jioni, baada ya msako wa saa moja ndani na karibu na bustani ya Highland Park.

Kisa hicho ndicho cha hivi karibuni zaidi, cha ufyatuaji risasi kiholela, ambao umesababisha vifo hapa Marekani, jambo ambalo limendelea kulaaniwa, huku baadhi ya wamarekani wakishutumu watunga sheria kwa kutoimarisha kanuni za umiliki wa bunduki, nuifanya vigumu kwa raia wa kawaida kupata silaha nzito kwa urahisi.

Shule, makanisa, maduka, na sasa gwaride za kijamii, zote zimekuwa maeneo ya mauaji katika miezi ya hivi karibuni.

Rais wa Marekani Joe Biden ametoa taarifa ya kulaani shambulizi hilo, akisema; “Mimi na mke wangu Jill tumeshtushwa na vurugu zisizo na maana za ufyatuaji risasi ambazo zimeleta huzuni tena kwa jamii moja ya Marekani katika Siku ya kuadhimisha Uhuru,” alisema Biden.

XS
SM
MD
LG