Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 22:18

Wahouthi wa Yemen wapuuza wito wa Marekani wa sitisho la mashambulizi


Wanamgambo wa Kihouthi
Wanamgambo wa Kihouthi

Wanamgambo wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran kwa mara nyingine wamepuuza wito wa Marekani wa kusitisha mashambulizi ya njia za meli za kimataifa.

Jumanne, wanamgambo hao walirusha makombora sita ya kuzuia meli kutoka maeneo yanayodhibitiwa na Wahouthi wa Yemen hadi Bahari ya Sham, afisa mmoja wa Marekani ameiambia Sauti ya Amerika.

Afisa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema wanajeshi wa majini wa Marekani walifyatua angalau moja ya makombora siku ya Jumanne, huku mengine yakiangukia baharini.

Kulingana na kampuni ya usalama ya Uingereza ya Ambrey, moja ya silaha za Wahouthi zilisababisha uharibifu mdogo kwa meli ya mizigo inayokuwa na bendera ya Barbados, lakini inayomilikiwa na Uingereza, wakati wa mashambulizi ya Jumanne.

Naibu msemaji wa Pentagon Sabrina Singh alithibitishia waandishi wa habari kwamba Wahouthi walikuwa wamefanya mashambulizi zaidi, lakini hakutoa maelezo zaidi.

Saa chache kabla ya hayo, jeshi la Marekani lilikuwa limeshambuzli ndege mbili zisizo na rubani, aina ya Kamikaze, ambazo zilijaa vilipuzi.

Forum

XS
SM
MD
LG