Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 23:36

Djibout yaimarisha ulinzi katika bahari ya Shamu


Boti ya Jeshi la Wanamaji wa Ujerumani katika bandari ya Djibouti. Picha na Reuters
Boti ya Jeshi la Wanamaji wa Ujerumani katika bandari ya Djibouti. Picha na Reuters

Taifa la Pembe mwa Afrika Djibout limeimarisha doria za ulinzi wa mwambao katika maeneo yake muhimu ya kijeshi baharini wakati mzozo katika bahari ya Sham umesababisha serikali katika kanda hiyo kuhakikisha hali haiwezi kuenea katika nchi zao.

Njia nyembamba ya Bab al- Mandab ndio pekee inayotenganisha Djibout na Yemen ambapo kundi la wanamgambo wa Houthi linafanya mfululizo wa mashambulizi dhidi ya meli zenye uhusiano na Israel tangu mwezi Novemba katika kile inachosema ni sehemu ya kulipiza kisasi dhidi ya ghasia za Gaza.

Wakati Duniani inafuatilia kwa karibu hali ilivyo hasa kwa kuzingatia umuhimu wa njia hiyo ya bahari inayotumika kwa biashara ya kimataifa inaunganisha Asia, Ulaya, na Afrika , taifa dogo la Djibout lililoko katika pembe ya Afrika linashuhudia sehemu kubwa ya mivutano inayojitokeza.

Nchi hiyo imefanikiwa kiuchumi katika muongo uliopita, lakini wakati mzozo unaonedelea unatishia ukuaji huo, na kusababisha maafisa wa kikosi cha ulinzi wa pwani kuongeza Doria huku wakitarajia kuimarisha usalama wa bahari na kuzuiya usumbufu wowote mkubwa.

Forum

XS
SM
MD
LG