Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 00:46

Tunaunga mkono Somalia kupinga mkataba wa Ethiopia na Somaliland - Rais wa Misri


Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi.
Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi.

Kiongozi wa Misri alisema Jumapili kuwa nchi yake Inashirikiana bega kwa bega na Somalia katika mzozo wake na Ethiopia, isiyo na bandari, ambayo ilifikia makubaliano na Somaliland kuiwezesha kufikia bahari ya Sham na kuanzisha kituo cha jeshi la majini.

Rais Abdel Fattah el-Sissi alikosoa makubaliano ya Ethiopia na eneo lililojitenga na kutoa wito kwa Ethiopia kutumia bandari za Somalia na Djibouti "kupitia nchi zingine," badala ya kujaribu kufanya kile alichokiita "kudhibiti eneo la nchi nyingine."

"Hatutaruhusu mtu yeyote kutishia Somalia au kuingilia ardhi yake," el-Sissi aliuambia mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari mjini Cairo, akiandamana na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud.

“Hakuna mtu anayepaswa kujaribu kuwatisha ndugu wa Misri, hasa ikiwa ndugu zetu watatuomba tushirikiane nao,” alisema.

Somaliland, eneo ambalo liko kimkakati karibu na Ghuba ya Aden, lilijitenga na Somalia mwaka 1991 wakati nchi hiyo ilipotumbukia katika mzozo ulioongozwa na wababe wa kivita. Eneo hilo limedumisha serikali yake licha ya kukosa kutambuliwa kimataifa.

Kiongozi wa Somaliland Muse Bihi Abdi alitia saini mkataba wa maelewano na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed mapema mwezi huu ili kuruhusu Ethiopia kukodisha ukanda wa pwani wa kilomita 20 ili kuanzisha kituo cha jeshi la wanamaji.

Forum

XS
SM
MD
LG