Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 01:47

Russia, China zaishutumu Marekani kwa "kuchochea taharuki Mashariki ya Kati"


Rais wa Russia Vladimir Putin.
Rais wa Russia Vladimir Putin.

Russia na China ziliilaumu Marekani wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu kwa kuchochea hali ya wasiwasi katika Mashariki ya Kati.

Matamshi hayo yanatokana na mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani ya kulipiza kisasi, dhidi ya makundi yanayoungwa mkono na Iran, nchini Iraq na Syria.

Jeshi la Marekani lilishambulia maeneo kadhaa nchini Syria na Iraq mwishoni mwa wiki, kulipiza kisasi shambulio la Januari 28, kwenye kambi ya kijeshi, nchini Jordan lililoua wanajeshi watatu wa Marekani.

Jumatatu, balozi wa China Jun Zhang vile vile alidai kuwa "vitendo vya Marekani bila shaka vitazidisha mzunguko mbaya wa vurugu za kulipiza kisasi katika Mashariki ya Kati."

Mashambulizi hayo ambayo yalilenga makundi ya wapiganaji wanaoiunga mkono Iran, yamesababisha hofu kwamba vita vinavyoendelea kati ya Israel na Hamas huko Gaza vinaweza kuzua mzozo wa kikanda.

"Ni wazi kwamba mashambulizi ya anga ya Marekani yanalenga kwa makusudi kuzua mzozo," alisema balozi wa Russia, Vasily Nebe-nzia, ambaye nchi yake iliitisha mkutano huo wa dharura.

Gadhabu kuhusu mashambulizi ya Israel huko Gaza -- yaliyoanza baada ya shambulio lililotekelezwa na wanamgambo wa Hamas tarehe 7 mwezi oktoba mwaka jana - imeongezeka katika Mashariki ya Kati, na kuchochea ghasia zilizohusisha makundi yanayoungwa mkono na Iran huko Lebanon, Iraq, Syria na Yemen.

Forum

XS
SM
MD
LG