Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:33

Wahadhiri, madaktari bingwa, wafanyakazi wagoma Kenya


Mandera County, Kenya
Mandera County, Kenya

Masomo katika vyuo vikuu vya serikali na vyuo vya udaktari yalisimama Alhamisi baada ya wahadhiri na wafanyakazi wa vyuo hivyo na madaktari bingwa kugoma wakidai marekebisho ya muundo wa mishahara.

Vyanzo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa wanachama wa umoja wa wahadhiri vyuo vikuu (Uasu), Umoja wa wafanyakazi wa vyuo vikuu Kenya (Kusu), Kudheiha na Umoja wa Wataalamu wa Afya na madaktari wa meno (KMPDU) wameapa kutorejea kazini mpaka pale serikali itakapokubaliana kuonyesha pendekezo lake kujibu pendekezo lao la muundo wa mishahara walilolitoa 2017-2021.

Kwa mujibu wa gazeti la The Nation waandamanaji hao vinginevyo, wanataka muajiri wao aheshimu na kutekeleza pendekezo lao kama lilivyotolewa.

Katibu mkuu wa Uasu Constantine Wasonga amesema walikuwa hawajapinga agizo la Waziri wa Fedha Ukur Yattani la kutoa fursa ya kuwepo mazungumzo kufikia suluhu.

“Sisi hatujawahi kukataa kukutana na msuluhishi, badala yake anatakiwa kuyafahamisha mabaraza ya vyuo na serikali kupeleka mapendekezo yao, lakini sisi mgomo wetu unaanza rasmi leo ,” aliwaambia waandishi wa habari

XS
SM
MD
LG