Baada ya miaka miwili ambapo Warepublikan wamekuwa wakiidhibiti White House, Baraza la Seneti na Baraza la Wawakilishi, Wademokrat ndio walio wengi hivi sasa katika Baraza la Wawakilishi.
Wademokrat wachukuwa uongozi wa Bunge la Marekani - Congress
Utawala wa serikali ya Marekani uliyo gawanyika unarejea kazini Marekani Alhamisi wakati Bunge jipya la Marekani likiapishwa.
5
Mwakilishi Rashida Tlaib (D-MI), Mpalestina-Mmarekani wa kwanza kuchaguliwa kuingia katika Bunge akiwa na wananchi wanaomuunga mkono nje ya ofisi yake katika jengo la Longworth House Office Building (LHOB), Washington, D.C., Jan. 3, 2019.
6
Mwakilishi wa Alexandria Ocasio-Cortez (D-NY) akipiga picha ya selfie na mwakilishi Sheila Jackson Lee (D-TX) ndani ya bunge kabla ya kikao cha kuapishwa kuanza.
7
Kiongozi wa Wademokrat Nancy Pelosi wa California, ataye ongoza Bunge la Marekani - Congress katika kikao cha 116 kama spika, kiongozi wa walio wachache katika Baraza la Seneti Chuck Schumer wa New York, akiwa amesimama na spika katika ukumbi wa Bunge mjini Washington, Alhamisi, Jan. 3, 2019. (AP Photo/Carolyn Kaster)
8
Mwakilishi Eric Swalwell (D-CA) akimshikilia binti yake Kathryn wakati Bunge likiendesha kikao chake cha 116 Washington, Jan. 3, 2019.