Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 28, 2023 Local time: 22:21

Waandishi wa habari wa Myanmar waliokimbilia Thailand wanaishi kwa wasiwasi


Ramani ya Thailand ikionyesha maeneo ya miji mikubwa ya nchi hiyo.
Ramani ya Thailand ikionyesha maeneo ya miji mikubwa ya nchi hiyo.

Ni zaidi ya mwaka mmoja tangu jeshi la Myanmar lilipochukuwa madaraka katika mapinduzi yaliyopelekea maelfu ya watu kukimbia nchini humo.

Kati yao ni waandishi wa habari kadhaa wenye weledi ambao walitafuta hifadhi nchini Thailand.

Baadhi tangu wakati huo wameondoka au kwenda kuishi kwingineko, lakini wengine walibakia Thailand, wakiishi kwa hofu ya polisi kuwakamata au kuwarejesha Myanmar.

“Hadhi yao ya ukazi wa muda mrefu ni changamoto kubwa sana ya kuwa uhamishoni, wala haijalishi mahali gani wako,” mwandishi wa muda mrefu wa Myanmar Aung Naing Soe, hivi sasa anaishi Thailand, alisema katika mahojiano.

Juhudi kadhaa zimeanzishwa na jumuiya za vyombo vya habari nchini Thailand kwa ajili ya waandishi wa habari wanaotokea Myanmar, wakiwapa msaada wa kifedha na wa kisheria ili waweze kuendelea kuendesha operesheni zao za habari hapa, au angalau waepuke kusumbuliwa na mamlaka husika.

Aung Naing Soe, hata hivyo, ambaye ana uzoefu na waandishi walioko uhamishoni, alisema mengi yanaweza kufanywa.

“Itakuwa ni jambo jema endapo kuna taasisi zozote zinazoweza kuwasaidia kupata hadhi ya kisheria ya uhamiaji kwa kuwasaidia kupata ukaazi katika nchi ya tatu kuliko kuwasaidia kurejea kupitia mpaka wa Thailand-Myanmar kisheria,” alisema.

“Waandishi wengi wa Myanmar walioko uhamishoni hawana nyaraka halali hivyo wanahitaji kupumzika na pia msaada wa matibabu ya afya ya akili.”

Bila ya kujua nani atafuatia

Thailand imekuwa ni kituo kikuu na sehemu ya mpito kwa wale wanaokimbia ghasia huko Myanmar kwa miongo kadhaa. Mapinduzi ya mwaka jana yalileta wimbi jipya la wakimbizi, wakiwemo waandishi, licha ya wanaofuatilia kusema ni vigumu kusema wangapi bado wako nchini Thailand.

“Baadhi waliondoka mapema, kama Machi 2021,” Johanna Son, ambaye anaendesha Reporting ASEAN, mtandao unaofuatilia matukio ya haki za raia huko Myanmar na eneo hilo, alisema. “Wengine walijaribu kufanya iwezekane, baadhi waligundua kuwa haiwezekani au siyo busara kubakia na kubahatisha maisha yao.”

Chavarong Limpattamapanee, rais wa Baraza la Habari la Taifa la Thailand alikadiria kuwa waandishi wa habari takriban 180 waliokuwa wamekimbia mapinduzi mwaka 2021 wako Thailand, wengi wao wako kaskazini, katika maeneo ya mpakani kama vile Mae Sot.

“Na karibu wote kati yao wanaogopa sana, kugunduliwa na kukamatwa,” amesema.

Thailand haijasaini Mkataba wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa, ambao unazikataza serikali kuwarejesha wakimbizi katika nchi zao kama wanakabiliwa na vitisho kwa uhai wao.

“Wale walioingia Thailand kisheria na wanataka kubakia wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuendelea kuwa na hadhi ya kisheria,” Phil Robertson, naibu mkurugenzi wa shirika la Human Rights Watch, kitengo cha Asia, amesema. “Wakati wengine waliokuwa wamevuka kirahisi mpakani wanakabiliwa na vitisho vya kukamatwa kwa kuingia kinyume cha sheria, na kuna uwezekano wa kurejeshwa Myanmar, wakati wowote.

XS
SM
MD
LG