Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:49

Jeshi Myanmar lamfungulia Suu Kyi mashtaka mapya matano ya ufisadi


Aung San Suu Kyi
Aung San Suu Kyi

Utawala wa kijeshi Myanmar siku ya Ijumaa umemuongezea mashtaka mapya matano ya ufisadi dhidi ya mkuu wa chama cha National League aliyepinduliwa, Aung San Suu Kyi, kulingana na chanzo cha karibu na mahakama hiyo ya siri ambako kesi inasikilizwa, ikifanya idadi ya makosa ya uhalifu yanayomkabili kufikia 16.

Utawala wa kijeshi Myanmar siku ya Ijumaa umemuongezea mashtaka mapya matano ya ufisadi dhidi ya mkuu wa chama cha National League aliyepinduliwa, Aungu San Suu Kyi, kulingana na chanzo cha karibu na mahakama hiyo ya siri ambako kesi inasikilizwa, ikifanya idadi ya ya makosa ya uhalifu yanayomkabili kufikia 16.

Mashtaka hayo, ambayo pia yalifikishwa dhidi ya rais wa zamani Win Myint, yanahusiana na ununuzi na matumizi ya helikopta kutoka mfuko wa fedha za Maafa wa Taifa ili kusimamia shughuli za kuzuia maafa chini ya serikali ya NLD, chanzo cha mahakamani katika mji mkuu wa Naypyidaw kimeliambia shirika la habari la RFA la Myanmar, kwa masharti majina yao yasitajwe.

Timu ya mawakili wa Suu Kyi iliwasilisha maombi dhidi ya mashtaka hayo mapya Ijumaa na waliambiwa na mahakama kuwa itapitia maombi hayo Januari 21.

Wakati kesi inasikilizwa Ijumaa, mahakama ilisikia ushahidi wa Khin Mar Cho, Mkaguzi Mkuu wa mkoa wa Yangon, ambaye aliletwa na waendesha mashtaka wa utawala kuzungumzia makosa ya ufisadi.

Mapema wiki hii, mahakama hiyo ilimhukumu Suu Kyi kwenda jela miaka minne kwa kumiliki vifaa vya mawasiliano Walkie-talkies na kuvunja masharti ya COVID-19, na kuongeza hukumu kufikia kifungo cha miaka sita alichopewa na mahakama inayoendesha kesi kwa siri.

Disemba tarehe 6, Suu Kyi na Win Myint walihukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa uchochezi dhidi ya jeshi na miaka miwili kwa kuvunja masharti ya janga la corona, ambapo mkuu wa jeshi, Min Aung Hlaing alipunguza kifungo hicho na kuwaweka kuzuizini cha nyumbani kwa miaka miw.

Chanzo cha habari hii ni Radio Free Asia

XS
SM
MD
LG