Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 18:44

Upinzani wa silaha dhidi ya utawala wa kijeshi Myanmar unaendelea kupata nguvu


FILE - Kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi linalopambana na utawala wa kijeshi Myanmar. Kambi hiyo iko msituni huko Jimbo la Kayin, Myanmar, in Disemba 2021. (Picha na AP)
FILE - Kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi linalopambana na utawala wa kijeshi Myanmar. Kambi hiyo iko msituni huko Jimbo la Kayin, Myanmar, in Disemba 2021. (Picha na AP)

Upinzani wa silaha kwa utawala wa kijeshi wa Myanmar ambao ulikamata madaraka kwa nguvu kutoka kwa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia mwaka mmoja uliopita umeendelea kujiimarisha dhidi ya wimbi la mashambulizi ya kikatili katika miezi ya karibuni na huenda yakawa yanaendelea kupata nguvu, wachambuzi wamesema.

Kwa kuwa yamekita mizizi katika sehemu kubwa za ndani ya nchi hiyo, wachambuzi hao wanaongezea, vikosi vya upinzani vimeanza kuweka shinikizo kwa jeshi lililoelemewa katika baadhi ya miji na majiji pia.

“Jeshi hilo linalazimika kupigana siyo tu nje ya miji; lakini inabidi wapigane kuzunguka sehemu za mijini,” amesema Matthew Arnold, mchambuzi wa kujitegemea anayefuatilia ghasia za baada ya mapinduzi huko Myanmar.

Ikijiimarisha kwa msako mkali wa umwagaji damu unaofanywa na jeshi kwa maandamano makubwa ambayo yalikabiliwa na mapinduzi ya Februari 2021, miji na maeneo jirani nchini kote yamekuwa yakiungana, wengi wakiwa na silaha na vilipuzi, kuupinga utawala wa kijeshi uliochukua madaraka kwa nguvu. Angalau wanamgambo 350, wanaoitwa majeshi ya ulinzi ya wananchi, au PDFs, wamejitangaza tangu jeshi kufanya mapinduzi.

Vita endelevu

Hata wanaofuatilia vipindi fulani Myanmar wanahangaika kufahamu ukubwa wa vita vya msituni vinavyoendeshwa na wengi walioko mbali na vikosi vilivyogawanyika wakiwa na machache lakini sababu za pamoja kuwaunganisha.

Wanasema wengi wa PDFs inawezekana siyo zaidi ya vikundi vya Facebook. Wengine wanakuja na kuondoka au kuungana, na kuendesha mapambano kutoka katika vituo vya nusu darzeni ya wapiganaji mijini wakiweka vilipuzi vilivyotengenezwa majumbani na vikundi vya wapiganaji 1,000 au wapiganaji zaidi walioenea maeneo makubwa ya milimani.

Kutaja idadi ya wanaoupinga utawala wa kijeshi ni “kama hiawezekani” amesema Anthony Davis, mchambuzi wa mambo ya usalama anayeishi Bangkok anayefanya kazi na wachapishaji wa majarida ya Janes defense.

“Lakini hakutakuwa na swali juu ya mamilioni ya watu kuwa wanaunga mkono harakati za PDF ambayo bila shaka inaonekana imejizatiti katika baadhi ya maeneo inawezekana inaongezeka,” aliongeza kueleza.

Vitongoji 330 Myanmar

Kati ya vitongoji 330 ya Myanmar, zaidi ya 250 vimeshuhudia upinzani wa kutumia silaha tangu mapinduzi yalipotokea, amesema Arnold, na angalau miji 150- takriban nusu yake – imekuwa na vita vinavyoendelea.

“Kwangu habari muhimu zaidi katika suala hili lote kwa hakika kumekuwa na athari ya kile unachoweza kukiita kujikita, ambapo vita vimejikita kwa hakika katika sehemu kubwa kwenye vitongoji kwenye baadhi ya maeneo,” amesema mchambuzi huyo.

Katika maeneo ya mipaka ya Myanmar, na India upande wa magharibi na China na Thailand upande wa mashariki, PDFs wanajikusanya na makabila ya walio wachache – wakiongozwa na waasi wenye silaha ambao wamekuwa wakipigana na jeshi hilo kutaka kujitawala kwa miongo mingi, wakitumia uzoefu wao wa vita vya msituni na, kwa uangalifu zaidi, na silaha mbalimbali.

XS
SM
MD
LG