Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 02:40

Waafghanistan wapoteza ajira, waangukia katika umaskini, njaa


Waafghanistan wakiangukia katika umaskini. Wanawake wakiwa katika mstari kupokea msaada wa fedha ili wheeze kujikimu kimaisha, ulioandaliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, mjini Kabul, Afghanistan, Saturday, Nov. 20, 2021(AP Photo/Petros Giannakouris)
Waafghanistan wakiangukia katika umaskini. Wanawake wakiwa katika mstari kupokea msaada wa fedha ili wheeze kujikimu kimaisha, ulioandaliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, mjini Kabul, Afghanistan, Saturday, Nov. 20, 2021(AP Photo/Petros Giannakouris)

Mamia ya wanaume na wanawake walipanga mstari kwenye eneo la mazoezi magharibi mwa Kabul mwishoni mwa wiki ili kupatiwa mgao wa fedha kiasi cha hela za Afghanistan 7,000 kwa miezi miwili sawa na dola 76.

Familia nyingi za Afghanistan ambazo ziliwahi kuwa na uhakika wa mapato thabiti hivi sasa zimetumbukia katika hali ya kukata tamaa, kutokuwa na uhakika wa jinsi watakavyopata pesa kununua mlo wao.

Baada ya Taliban kuchukua udhibiti mwezi Agosti, dunia ilikata ufadhili kwa serikali na miradi mingi ya maendeleo, na kuwafanya watu wa daraja la kati ambao walikuwa kwa kiasi kikubwa wakitegemea ajira ambazo zilitokana na fedha kutoka nje kutokuwa na kazi.

Huku Umoja wa Mataifa ukitoa onyo kwa mamilioni ya watu ambao wanakaribia hali mbaya ya njaa, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani limezidisha kwa kiasi kikubwa misaada ya moja kwa moja kwa familia.

Mwaka 2020, shirika hilo la Mpango wa Chakula Duniani lilitoa msaada kwa takriban watu milioni tisa. Hadi hivi sasa mwaka 2021, idadi hiyo imeongezeka na kufikia takriban milioni 14. Mwaka 2022, shirika hilo linalenga kutoa msaada kwa zaidi ya watu milioni 23 na kusema litahitaji kiasi cha dola kilioni 220 kwa mwezi kufanya hivyo.

Shirika na maendeleo la Umoja wa Mataifa, shirika la Afya duniani na UNICEF wanafanya kazi moja kwa moja katika kuwalipa mishahara madaktari na wauguzi kote nchini ili kuhakikisha sekta ya afya haianguki. WFP, wakati huo inatoa msaada wa fedha taslimu moja kwa moja na chakula kwa familia kujaribu kuwasaidia wasiwe katika hali mbaya kimaisha.

XS
SM
MD
LG