Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 07:51

Taliban yapiga marufuku televisheni Afghanistan kuonyesha tamthilia zinazo shirikisha wasanii wa kike


Utawala wa Taliban nchini Afghanistan, Jumapili umetoa amri kwa vituo vya televisheni nchini Afghanistan kuacha kurusha tamthilia zikionyesha wasanii wa kike.

Amri hiyo pia inawataka wanahabari wanawake kuvaa hijabu kwa mujibu wa kundi hilo ambalo limetafsiri sheria za kislamu.

Marufuku hiyo ni miongoni mwa miongozo nane iliyo tolewa na wizara moja ya serekali ya Taliban ikiwa ni moja ya ishara ya kwamba kundi hilo linaweka masharti kwa haki za wanawake.

Pia kanuni hizo zinaeleza kwamba filamu na tamthilia hazipaswi kuwashirikisha waigizaji wa kike.

Kwa kuongeza, sera hiyo mpya inakataza vituo vya televisheni kuonyesha wanaume ambao wanaonekana kutojifunika vizuri kwa kutoonyesha wale wanao onekana kuanzia kufuani mpaka magotini.

XS
SM
MD
LG