Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:01

Mamilioni ya watu kukabiliwa na njaa Afghanistan - WFP


Mto akisubiri mgao wa chakula Afghanistan. Picha na REUTERS/Omar
Mto akisubiri mgao wa chakula Afghanistan. Picha na REUTERS/Omar

Shirika la chakula duniani -WFP- limesema mamilioni ya raia wa Afghanistan watakabiliwa na njaa wakati wa kipindi cha majira ya baridi kama hatua za haraka hazitachukuliwa.

Nusu ya watu wote nchini humo ambao ni takriban milioni 22.8 wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula wakati milioni 3.2 ni Watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, wanaweza kukumbwa na utapiamlo mkubwa, WFP imeongeza kusema.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo David Beasley amesema wanaona kuna janga mbele yao.

Afghanistan ilitumbukia katika utawala wa kundi la Taliban mwezi Augusti baada ya Marekani kuondoa vikosi vyake vya mwisho na wanamgambo wakaingia katika miji kuchukua udhibiti.

Udhibiti wa Taliban umedhoofisha uchumi ambao tayari ulikuwa tete ukitegemea zaidi msaada wa kigeni.

Mataifa ya magharibi yamesitisha misaada yake na mashirika ya benki ya dunia na IMF pia yameacha kutoa fedha kwa nchi hiyo.

Taifa linaonekana kuwa linategemea msaada wakati asilimia 10 ya pato lake la ndani linategemea msaada wa kigeni.

Kwa kesi ya afghanistani taktiban asilimia 40 ya pato lake linatokana na msaada wa kimataifa, kwa mujibu wa benki ya duniani.

XS
SM
MD
LG