Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 13:22

Ndege ya misaada ya UNHCR yatua Kabul


Ndege ikishusha misaada ya UN katika picha ya maktaba
Ndege ikishusha misaada ya UN katika picha ya maktaba

Ripoti kutoka makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswizi zinasema kwamba ndege iliyokodishwa na Umoja huo ikiwa imebeba vifaa muhimu vya kukabiliana na msimu wa baridi imeatua Jumanne kwenye uwanja wa ndege wa Kabul nchini Afghanistan. 

Hiyo ni moja ya ndege zilizo pangwa kusafirisha bidhaa kutoka kwenye ghala la UNHCR lililoko Dubai kuelekea Kabul wiki hii. Ndege iliyowasili ilkuwa imebeba tani 33 za bidhaa muhimu za kujikinga baridi. Ghasia pamoja na ukosefu wa usalama vimetorosha makwao takriban watu milioni 3.5 nchini Afghanistan wakiwemo takriban wakimbizi wapya 700,000 mwaka huu.


Msemaji wa UNHCR Shabia Mantoo amesema kwamba wanalenga kusiadia walau watu nusu milioni waliokoseshwa makao. Ameongeza kusema kwamba UNHCR inaharakisha kutoa misaada yake kabla ya msimu wa baridi kali kuingia na kuwa vigumu kufikisha misaada. Inasemekana kwamba tayari hali hiyo imeanza kushuhudiwa wakati baadhi ya sehemu zikiwa na viwango vya baridi ya chini ya degree sifuri nyakati za usiku.

XS
SM
MD
LG