Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 12:29

Vyuo 19 Tanzania vyafutiwa udahili na TCU


Nembo ya TCU

Vyuo 19 nchini Tanzania vimefutiwa udahili na Tume ya Vyuo vikuu (TCU).

Pia TCU imefuta kozi 75 katika vyuo 22 kwa sababu ya kukiuka Sheria, taratibu na kanuni za utoaji wa elimu ya juu hapa nchini.

Afisa Habari wa Tume Edward Mkaku amesema uamuzi wa kuvifutia udahili baadhi ya vyuo ni kutekeleza agizo la serikali lililoitaka tasisi hiyo kuvisimamia kwa karibu vyuo ili viweze kutoa elimu bora.

Ameongeza kusema kuwa vyuo ambavyo wanafunzi wanaendelea na masomo mabadiliko haya hayatawahusu wanafunzi waliopo, isipokuwa vyuo hivyo havitaruhusiwa kudahili wanafunzi wapya kwa mwaka huu wa masomo.

Pia baadhi ya sababu za vyuo hivyo kufutiwa udahili wa Shahada, Shahada za Uzamili pamoja na Shahada za Uzamivu kuwa ni kukosa vitendeakazi na wataalamu katika kufundisha elimu ya juu.

Alivitaja baadhi ya vyuo vinavyotoa taaluma za afya kama Kilimanjaro Christian Medical College (KCMC) cha mkoani Kilimanjaro, Kampala International University (KIU) na Hubert Kairuki Memorial University (HKMU) vya Jijini Dar es Salaam ambavyo vilikuwa vikitoa kozi za udaktari, ufamasia pamoja na shahada ya uzamili katika Udaktari wa magonjwa ya wanawake iliyokuwa ikitolewa na Chuo cha Hubert Kairuki imebainika kuwa hawakuwa na vifaa na wataalamu wa kutosha kufundisha kozi hizo.

Vyuo vingine ni St. Joseph, St. John, Tumaini University pamoja na vyuo vingine kadhaa ambavyo havina waalimu pamoja na vifaa kwa mujibu wa maelekezo ya Tume hiyo.


Facebook Forum

XS
SM
MD
LG