Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 06, 2022 Local time: 01:23

Vyama vya kisiasa vyapinga kuongezwa kwa muda wa mpito Mali


Kiongozi wa kijeshi wa Mali Kanali. Assimi Goita,

Muungano wa vyama vya kisiasa nchini Mali Jumanne umepinga mpango uliotangazwa awali na serikali ya kijeshi kwamba ingechukua hadi miaka mitano ya mpito kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika.

Mali imekuwa chini ya shinikizo kutoka mataifa ya Afrika Magharibi la kuitisha uchaguzi tangu kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi mwezi Mei, yakiwa ya pili ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Viongozi wa kijeshi wa Mali siku chache zilizopita wametoa waraka mpya kwa muungano wa kibiashara wa mataifa ya Afrika magharibi ,ECOWAS, ukipendekeza mpango wa miaka mitano kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais hapo mwaka wa 2026.

Mwanzoni kipindi cha mpito kilikusudiwa kuchukua miezi 18 baada ya mapinduzi ya kijeshi yalioongozwa na rais wa sasa Assimi Goita, na kumuondoa madarakani rais Ibrahim Boubacar Keita hapo Agosti 2020. Mpango wa kwanza ulikuwa kwamba uchaguzi ufanyike Februari mwaka huu.

Hata hivyo muungano wa vyama vya kisiasa umetoa waraka wa kupinga hatua hiyo, huku ukisusia mashauriano ya kitaifa yaliochukua siku 4, ukisema kwamba yaliitishwa ili serikali iweze kuongeza muda wa mpito. Msemaji wa muungano huo Amadou Koita anasema kwamba wanaomba viongozi wa kijeshi walio madarakani kuheshimu mchakato wa mpito uliowekwa.

Hivi karibuni Ufaransa iliondoa vikosi vyake nchini humo ikibakisha kambi moja tu upande wa kaskazini. ECOWAS kwa upande wake imetishia kuongeza vikwazo dhidi ya Mali iwapo utawala ulioko wa kijeshi hautaheshimu tarehe ya uchaguzi iliyowekwa ya mwezi Februari mwaka huu. Rais wa Ghana Nana Akufo Addo ambaye pia ni mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS anatarajiwa kuzulu Mali Jumatano ili kushauriana kuhusu ratiba ya mpito. Mkutano wa ECOWAS kwa ajili ya Mali pia umepangwa kufanyika Jumapili mjini Accra.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG