Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 09:54

Chad inapanga kupeleka wanajeshi 1,000 wa ziada nchini Mali

Wanajeshi wa Chad wakiwa katika soko la Koundoul kilometa 25 kutoka N'Djamena, Jan. 3, 2020.

Wizara ya mambo ya nje ya Mali imesema kuwa Chad inapanga kupeleka wanajeshi 1,000 wa ziada nchini Mali ili kuwaongezea nguvu wanajeshi wake wanaopambana na waasi huko, huku Ufaransa ikipunguza majeshi yake  katika eneo la Sahel barani Afrika.

Wanajeshi wa Chad ni takriban 1,400 kati ya wanajeshi 13,000 wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani kaskazini na katikati mwa Mali, ambako uasi wa Kiislamu umeshamiri licha ya juhudi za miaka tisa za majeshi ya kimataifa kuudhibiti.

Kupelekwa huko kwa wanajeshi kunakotarajiwa kuimarisha wanajeshi hao na wengine wa Chad wakati mtawala wa zamani wa kikoloni Ufaransa akipunguza kiwango wanajeshi wake hadi 5,000 wa kikanda ili kukabiliana na ugaidi unaojulikana kama Barkhane, wizara ya mambo ya nje ya Mali ilisema katika taarifa yake siku ya Ijumaa.

Kutumwa huko ni sehemu ya mpango wa nchi mbili kwa ombi la Serikali ya Chad kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake Kaskazini mwa Mali kufuatia uundaji upya wa kikosi cha Barkhane wizara hiyo ilisema katika taarifa yake.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG