Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 14:59

Viongozi wa Taliban waamuru shule za wasichana kufungwa


FILE - Wanafunzi wa kike wakiondoka katika shule ya msingi Kabul, Afghanistan, Machi 27, 2021. (AP Photo/Rahmat Gul, File)
FILE - Wanafunzi wa kike wakiondoka katika shule ya msingi Kabul, Afghanistan, Machi 27, 2021. (AP Photo/Rahmat Gul, File)

Wasichana nchini Aghanistan waliokuwa wameripoti shuleni kwa mara ya kwanza tangu mwezi Agosti mwaka uliyopita wameamriwa kurudi nyumbani saa chache baada ya kuingia madarasani.

Kundi la Taliban liliamuru wasichana katika shule za upili nchini Afghanistan kuondoka shuleni muda mfupi walipoingia madarasani na kupelekea wasiwasi kuhusu msimamo mkali wa kundi hilo la Kiislamu.

Msemaji wa Taliban Inamullah Samangani ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wanafunzi wasichana wameamriwa kurudi nyumbani.

Waandishi wa habari wa AFP walishuhudia wanafunzi hao wakiambiwa waondoke shule na kurudi nyumbani.

Wasichana hao walionekana wakidondokwa machozi wakati wanapakia mizigo yao na kuondoka.

Jamii ya kimataifa imesema kwamba elimu ni haki ya kila mtu na kufanya haki hiyo kuwa suala muhimu katika mazungumzo ya kutoa msaada na kutambua utawala wa Taliban.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG