Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 05:38

Viongozi wa dunia waomboleza kifo cha Prince Philip

Maua nje ya Kasri ya Windsor kuomboleza kifo cha Prince Philip wa Uingereza, mume wa Malkia Elizabeth, aliyekufa akiwa na miaka 99, huko Windsor, karibu na London, Uingereza, Aprili 9, 2021. REUTERS/Andrew Boyers

Wafalme, wakuu wa nchi na mawaziri wakuu kote duniani, waliopo madarakani na wa zamani wametuma salaam za rambi rambi kufuatia kifo cha Prince Philip, wa Uingereza akiwa na umri wa miaka 99.

Mfalme na Malkia wa Spain walituma ujumbe wa telegram wakisema Mpenzi Shangazi Lilibet tunaomboleza kifo cha “Mpenzi Mjomba Phillip.”

Rais wa Marekani Joe Biden alituma salaam akisema Prince Phillip aliyekuwa na umri wa miaka 99 hakuwahi kupunguza kasi ya shughuli zake hata kidogo. Marais wote wa zamani wa marekani pia wametumba rambi rambi zao.

Bendera zilishushwa nusu mlingoti katika bunge la Australia mjini Canberra.

Na viongozi wa Afrika ikiwemo Zimbabwe, ambaye imekuwa na uhusiano usio mzuri na Uingereza pia imetuma salaam na Rais wa Tanzania naye alituma rambi rambi.

​
XS
SM
MD
LG