Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 11:08

Mahakama Kenya yasitisha kufungwa kwa kambi za wakimbizi


Mkimbizi wa Somalia Fatuma Yussuf Diriye akihojiwa na shirika la habari la Uingereza Reuters katika kambi ya Kakuma kaskazini mea Kenya, Agosti. 13, 2018.
Mkimbizi wa Somalia Fatuma Yussuf Diriye akihojiwa na shirika la habari la Uingereza Reuters katika kambi ya Kakuma kaskazini mea Kenya, Agosti. 13, 2018.

Mahakama Kuu ya Kenya imesitisha hatua ya serikali nchini humo kufunga kambi mbili za wakimbizi ambazo zinahifadhi maelfu ya wakimbizi kutoka nchi Jirani zilizokumbwa na vita.

Jaji Antony Mirima alitoa agizo la muda hapo Alhamis baada ya aliyekuwa mgombea urais Peter Gichira kuwasilisha changamoto ya kisheria kutaka kuzuia kufungwa kwa kambi mbili za wakimbizi.

Wizara ya mambo ya ndani Kenya ilikuwa imewapa idara ya kuhudumia wakimbizi ya Umoja wa Mataifa-UNHCR hadi Jumatano kubuni mpango wa kufunga kambi hizo.

Kambi ya Dadaab iliyopo mashariki mwa Kenya inahifadhi zaidi ya wakimbizi laki mbili, wengi kutoka Somalia ambayo imekuwa kwenye machafuko kwa miongo kadhaa.

Kambi ya Kakuma iliyopo kaskazini mwa Kenya inahifadhi wakimbizi takribani laki mbili na wale wanaotafuta hifadhi, wengi kutoka Sudan Kusini ambao wanapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.

XS
SM
MD
LG