Pia wanafamilia walijitokeza kwa wingi kuja kushuhudia na kusheherekea kuokolewa kwa vijana hao ambalo ni tukio la kihistoria.
Vijana waliookolewa Thailand waendelea vizuri na matibabu
Wanafunzi, viongozi wa dini ya Buddha walijitokeza kufanya maombi maalum kwa vijana 12 na kocha wao. Wanafunzi walifanya maombi katika shule ya Maesaiprasitsart ambapo vijana sita kati ya kumi na mbili wanasoma na wote wako katika furaha baada ya kuokolewa kwa wanafunzi wenzao.
5
Wanafamilia wakipongezana baada ya kusikia habari za faraja za kupatikana kwa vijana 12 na kocha wao katika pnago la Mae Sai lililokuwa limefurika huko Thailand, Julai 2, 2018.
6
Wanajeshi wa majini wa Thai walipofanikiwa kumtoa kijana kutoka katika pango la Tham Luang Nang huko Mae Sai, jimbo la Chaing Rai, kaskazini mwa Thailand.
7
Wanafunzi wakisheherekea kuokolewa kwa vijana 12 na kocha wao mbele ya hospitali ambapo vijana hao wanaendelea na matibabu, Julai 11, 2018.