Pia wanafamilia walijitokeza kwa wingi kuja kushuhudia na kusheherekea kuokolewa kwa vijana hao ambalo ni tukio la kihistoria.
Vijana waliookolewa Thailand waendelea vizuri na matibabu
Wanafunzi, viongozi wa dini ya Buddha walijitokeza kufanya maombi maalum kwa vijana 12 na kocha wao. Wanafunzi walifanya maombi katika shule ya Maesaiprasitsart ambapo vijana sita kati ya kumi na mbili wanasoma na wote wako katika furaha baada ya kuokolewa kwa wanafunzi wenzao.

1
Wanafunzi wakifanya maombi katika shule ya Maesaiprasitsart ambapo vijana sita kati ya kumi na mbili wanasoma na wote wanafurahia kuokolewa kwa wanafunzi wenzao huko wilaya ya Mae Sai jimbo la Chiang Rai, kaskazini mwa Thailand, Jumatano, Julai 11, 2018.

2
Baadhi ya wanafamilia wakishuhudia vijana walio okolewa katika dirisha nje ya wodi ambapo wamelazwa na wanaendelea kupata nafuu katika hospitali ya Chiang Rai huko Jimbo la Chiang Rai Jumatano, Julai 11, 2018.

3
Vijana watatu kati ya 12 wakiwa wamepata afueni wakati wanaendelea kupata matibabu hospitalini baada ya kuokolewa pamoja na kocha wao kutoka katika pango lililokuwa limekumbwa na mafuriko huko Mae Sai, Jimbo la Chiang Rai upande wa kaskazini mwa Thailand.

4
FILE - Viongozi wa kiroho wa dhehebu la Buddha wakiwaombea vijana 12 na kocha wao huko Mae Sai, Jimbo la Chiang Rai, Kaskazini mwa Thailand, Juni 27, 2018.