Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 14:23

Utawala wa Kijeshi Mali waahirisha uchaguzi wa rais


Kiongozi wa serikali ya mpito na kiongozi wa jeshi la Mali Kanali Assimi Goïta (Kulia) akiwa na kiongozi wa serikali ya mpito na mkuu wa majeshi wa Guinea, Mamady Doumbouya (kushoto) huko Bamako, Mali Septemba 22, 2022. Picha na OUSMANE MAKAVELI/AFP.
Kiongozi wa serikali ya mpito na kiongozi wa jeshi la Mali Kanali Assimi Goïta (Kulia) akiwa na kiongozi wa serikali ya mpito na mkuu wa majeshi wa Guinea, Mamady Doumbouya (kushoto) huko Bamako, Mali Septemba 22, 2022. Picha na OUSMANE MAKAVELI/AFP.

Utawala wa kijeshi nchi Mali umetangaza Jumatatu kuahirisha uchaguzi wa rais wenye lengo la kurejesha madaraka kwa raia wa taifa hilo la Afrika Magharibi lililokumbwa na wanajihadi.

Uchaguzi huo ambao ulitarajiwa kufanyika mwezi Februari umetangazwa kuahirishwa kutokana na sababu za kiufundi, jeshi limeahidi kutoa ratiba mpya baadaye.

Duru mbili za upigaji kura – awali zilipangwa kufanyika Febaruari 4 na 18, 2024 -- "zitaahirishwa kidogo kwa sababu za kiufundi" msemaji wa serikali, Abdoulaye Maiga alisema katika taarifa yake iliyosomwa kwa waandishi wa habari.

Sababu hizo ni pamoja na masuala yanayohusiana na kupitishwa kwa katiba mpya mwaka huu na tathmini ya orodha ya wapiga kura, alisema.

Pia msemaji huyo alielezea mzozo na kampuni ya Ufaransa ya Idemia, ambayo utawala wa kijeshi inasema inahusika katika mchakato wa sensa.

"Tarehe mpya za uchaguzi wa urais zitawasilishwa baadaye," alisema Maiga.

Mamlaka pia zinakataa kuandaa uchaguzi wa wabunge, uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2023, kabla ya uchaguzi wa rais.

Utawala wa kijeshi "umeamua kuandaa, uchaguzi wa rais peke yake ", ilisema taarifa hiyo.

Kiongozi wa serikali ya mpito, Kanali Assimi Goita (katikati) akiwa na wajumbe wa Mahakama kuu huko Bamako Juni 7, 2021. Picha na ANNIE RISEMBERG / AFP.
Kiongozi wa serikali ya mpito, Kanali Assimi Goita (katikati) akiwa na wajumbe wa Mahakama kuu huko Bamako Juni 7, 2021. Picha na ANNIE RISEMBERG / AFP.

Chaguzi nyingine zitafanyika kwa ratiba "iliyowekwa na mamlaka mpya, chini ya maagizo ya rais mpya".

Kuahirishwa huko ni uchelewesho mwingine wa ratiba ya utawala ya kukabidhi madaraka kwa viongozi wa kiraia waliochaguliwa.

Wanajeshi ambao walifanya mapinduzi yaliyofuatana kati ya mwaka 2020 na 2021, hapo awali waliahidi kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge mwezi Februari 2022.

Lakini utawala wa kijeshi, unaoongozwa na Assimi Goita, ulitangaza mwishoni mwa 2021 kwamba huikuweza kuheshimu ratiba iliyokubaliwa na kambi ya kikanda ya ECOWAS.

Na kusema kuwa utawala huo wa kijeshi unahitaji muda zaidi kufanya mabadiliko ya kina.

ECOWAS ilijibu mwanzoni mwa mwaka 2022 kwa kuiwekea Mali vikwazo vikali, hivyo kuiathiri vibaya nchi hiyo maskini na isiyo na bahari.

Taarifa ya Jumatatu haikutaja maendeleo ya hivi karibuni ya kiusalama, ikisema tu kwamba kiongozi wa kijeshi, Goita ana azma ya "kurejesha misingi ya katiba kwa amani na usalama, baada ya kufanya mabadiliko ya taatisi za kisiasa yanayoipa kipaumbele".

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP na Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG