Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 10:51

Ushoga waharamishwa Uganda


Mwanachama wa jumuiya ya watu waliobadili jinsia na LGBTQ huko Kampala, Uganda, Novemba 23, 2019. Picha na Sumy SADRUNI / AFP.
Mwanachama wa jumuiya ya watu waliobadili jinsia na LGBTQ huko Kampala, Uganda, Novemba 23, 2019. Picha na Sumy SADRUNI / AFP.

Bunge la Uganda Jumanne limepitisha sheria inayoharamisha kujitambulisha kama LGBTQ, na kuzipa mamlaka madaraka mapana katika kuwalenga raia wa Uganda ambao tayari wanakabiliwa na ubaguzi wa kisheria na manyanyaso wanayofanyiwa na makundi ya watu.

Zaidi ya nchi 30 za Afrika, ikiwemo Uganda, tayari zimepiga marufuku mahusiano ya jinsia moja. Sheria mpya inaonekana ni ya kwanza kuwafanya wale watakao jitambulisha kama wasagaji, mashoga, jinsia mbili, na waliobadilisha jinsia (LGBTQ), kuwa wanavunjasheria kwa mujibu wa kundi la Human Rights Watch.

Wafuasi wa sheria mpya wanasema sheria hiyo inahitajika kuwaadhibu wanaojishughulisha na harakati za LGBTQ, ambazo wanasema zinatishia maadili ya kitamaduni ya kikonsevative na kidini katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Kwa kuongezea na mapenzi ya jinsia moja, sheria inapiga marufuku kuhamasisha na kuunga mkono ushoga ikiwemo njama za kujihusisha na ushoga.

Atakaye kiuka sheria hiyo ataadhibiwa vikali ikiwa ni pamoja na hukumu ya kifo kwa kile walicho kiita ushoga uliokithiri, na kifungo cha maisha jela kwa wale watakao patikana na tuhuma za kufanya ngono za kishoga. Kundi jingine ni wale watakaodaiwa kuhusika na ushoga uliokithiri na kufanya ngono na watoto walio na umri wa chini ya miaka 18 au wakati mhusika anayefanya kitendo hicho ana HIV miongoni mwa sababu nyingine, kwa mujibu wa sheria.

Mtafuta hifadhi kutoka Uganda akijifunika uso kwa mfuko wa karatasi ili kulinda utambulisho wake huko Boston, Massachusetts Juni 8, 2013. Picha na REUTERS/Jessica Rinaldi.
Mtafuta hifadhi kutoka Uganda akijifunika uso kwa mfuko wa karatasi ili kulinda utambulisho wake huko Boston, Massachusetts Juni 8, 2013. Picha na REUTERS/Jessica Rinaldi.

"Muumba wetu Mungu anafurahi (kuhusu) kile kinachotokea ... Ninauunga mkono mswaada huu ili kulinda mustakabali wa watoto wetu," alisema mbunge David Bahati wakati wa mjadala kuhusu mswaada huo.

"Hii inahusu uhuru wa taifa letu, hakuna mtu anayepaswa

kututisha, hakuna anayetutisha." mswaada wa sheria hiyo utapelekwa kwa rais Yoweri Museveni ambako utatiwa saini na kuwa sheria.

Museveni hajazungumzia pendekezo la mswaada wa sasa, lakini

kwa muda mrefu amekuwaaikipinga haki za LGBTQ na kutia saini sheria inayopinga LGBTQ mwaka 2013 ambayo nchi za Magharibi zililaani kabla ya mahakama ya ndani kuifuta kwa madai kuwa ulishindwa kufuata taratibu.

Mwezi huu, mamlaka ilimkamata mwalimu wa shule ya sekondari iliyoko wilaya ya Jinja, mashariki mwa nchi kwa tuhuma za "kuwaandaa wasichana wadogo katika vitendo vya ngono visivyo vya asili."

Baadaye mwalimu huyo alishtakiwa kwa utovu wa nidhamu na kuwekwa mahabusu akisubiri kesi yake kusikilizwa.

Jumatatu polisi walisema waliwakamata watu sita kwa

kutuhumiwa kuendesha mtandao ambao "ulihusika kikamilifu kuwaanda watoto wa kiume katika vitendo vya kulawiti."

XS
SM
MD
LG