Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 06:25

Ushindani mkali wajitokeza kwenye uchaguzi wa katikati ya mhula Marekani

Ushindani umekua mkali kwenye uchaguzi wa katikati ya mhula nchini Marekani, ikiwa ni vigumu kujua nani atachukua uwongozi kwenye bunge la taifa na magavana wa baadhi ya majimbo.

Uchaguzi wa katikati ya mhula ukiwa umeingia katika kipindi cha lala salama, ushindani wa viti vingi umeongezeka kuwahi kushuhudia kwa miongo mingi hapa Marekani.

Kawaida uchaguzi huu hauwavuti sana wapiga kura lakini kufuatana na maafisa wa uchaguzi ni kwamba idadi ya watu walokwisha piga kura za awali ni kubwa kuwahi kushuhudiwa. Kulingana na utafiti wa maoni ulofanywa na taasisi ya Gallup ni kwamba kuna karibu asili mia 54 za Wademokrats walopiga kura mapema mwaka huu ukilinganisha na mwaka 2010, na asili mia 32 ya Warepublican wamepiga kura kulingana na 23 mwaka 2010.

Wachunguzi wa mambo wanasema ushindani umetokana na sababu mbali mbali - kuanzia uchumi, uhuru wa kujiamulia kwa wanawake kutoa mimba, kutoamini mfumo wa uchaguzi na wagombea wasioamini matokeo ya uchaguzi kama anavyosimulia rais wa zamani Donald Trump, hadi ughali wa maisha.

Ushindani mkubwa wa nani atachukua udhibiti wa baraza la Seneti utategemea nani atashinda kiti cha Georgia, ingawa uchunguzi wa maoni unaonesha kwamba huwenda Warepublican wakaweza kuchukua udhibti wa baraza la wawakilishi.

Hali hiyo ikitokea wadadisi wa siasa wanasema itakua vigmu sana kwa Rais Joe Biden kuendelea na ajenda yake katika miaka miwili iliyombakia.


Pandisha zaidi

Makundi

XS
SM
MD
LG