Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 21:52

UN yaonya vita vya Russia na Ukraine vinaweza kudumaza uthabiti Afrika


FILE - Mifuko ya unga wa ngano ikiwa imejazana katika ghala huko Ibafo, Jimbo la Ogun kusini magharibi ya Nigeria March 15, 2022. Picha na AFP.
FILE - Mifuko ya unga wa ngano ikiwa imejazana katika ghala huko Ibafo, Jimbo la Ogun kusini magharibi ya Nigeria March 15, 2022. Picha na AFP.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameonya kuwa kupanda kwa bei za chakula, mafuta, mbolea na bidhaa nyingine kutokana na vita kati ya Russia na Ukraine kunaweza kuwa na athari kubwa sana kudumaza uthabiti  katika bara la Afrika.

Afrika bado inajikwamua kutoka katika athari za uchumi wa kijamii uliotokana na janga la COVID-19, ambalo limewatumbukiza baadhi ya watu milioni 50 katika umaskini uliokithiri. Bara hilo pia linakabiliana na migogoro iliyosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, vita, na vurugu za kisiasa.

Ukiongezea mchanganyiko huu mbaya sana hivi sasa ni vita nchini Ukraine.

Msimamizi msaidizi na mkurugenzi wa Afrika wa program ya maendeleo ya UN Ahunna Eziakonwa, alisema uvamizi wa Russia nchini Ukraine unaleta athari mbaya katika bara hilo.

“Mambo ambayo kwa hakika yanashangaza kwa bara hilo na mwamko mbaya ni namna gani linategemea – karibu asilimia 90 ya vyanzo vya nje kwa bidhaa za vile wanavyohitaji kuweza kufanya watu wake waishi. Chakula na dawa,” alisema mkuu huyo.

Eziakonwa alisema athari za kuongezeka kwa mfumuko wa bei kutokana na kupanda kwa bei za chakula, mafuta, mbolea na bidhaa nyingine hivi karibuni athari zake zitaanza kuonekana. Mwanamama huyo alisema utegemezi wa Afrika katika uagizaji chakula na bidhaa nyingine kutoka Russia na Ukraine utasababisha hali nyingine ya mashaka na uwezekano wa ghasia katika mataifa kadhaa.

Mchumi mwandamizi wa UNDP – Afrika Raymond Gilpin alisema kuongezeka kwa mfumuko wa bei kunawaweka idadi kadhaa ya wawekezaji wakubwa kutowekeza kote barani humo. Alitoa mifano kamaile ya uendelezaji wa viwanda vikubwa vya chuma huko Nigeria na mbolea huko Angola.

Golpin alionya mivutano inaongezeka katika maeneo yenye vita kama vile Sahel, baadhi ya sehemu za Afrika ya Kati, na Pembe ya Afrika wakati vita ya Russia na Ukraine vinapamba moto.

“Hususan katika maeneo ya mijini, jamii za kipato cha chini, hali inayoweza kupelekea katika maandamano ya ghasia na … pengine fujo zenye uharibifu,” alisema mchumi huyo.

Kadhalika na nchi kadhaa zilizopanga kuwa na uchaguzi mwaka huu na mwakani wako hatarini kwa sababu hili linaweza kuwa chanzo cha yote hayo.”

UNDP
UNDP

Maafisa wa UNDP wanatoa wito kuwepo hatua za kimataifa kutatua tatizo hili huko Afrika kutokana na hatua zilizochukuliwa na nusu ya dunia mbali na wao.

Wanasema matokeo ya muda mrefu ya mgogoro huu mpya duniani unakuwa ni tishio kubwa kwa juhudi za amani na utulivu katika bara hilo.

Hatari hizi, wanaeleza, zimekuja wakati nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara zinachangia karibu nusu ya vifo ulimwenguni vinavyosababishwa na ugaidi kama inavyoonekana katika rekodi za idadi ya mapinduzi mwaka jana.

XS
SM
MD
LG