Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 07:54

UN yakerwa na serikali Kenya kukaidi amri ya mahakama


Rupert Colville
Rupert Colville

Ofisi ya Kamishna wa Haki za Binadamu katika Umoja wa mataifa amekosoa hatua ya kuendelea kufungiwa vituo vitatu huru vya televisheni nchini Kenya licha ya uamuzi wa mahakama ukiitaka serikali kuondoa marufuku hiyo.

Msemaji wa haki za binadamu, Rupert Colville anasema ofisi ya Umoja wa Mataifa ina wasi wasi kwa serikali ya Kenya kukataa kuheshimu maamuzi ya Mahakama Kuu ya Kenya ya kuruhusu vituo hivyo vya televisheni kuanza tena kurusha matangazo yao. Anasema serikali ni budi iheshimu na kutekeleza maamuzi ya kisheria.

“Tuna wasi wasi pia na majaribio yake ya kuingilia kati haki ya uhuru wa kujieleza kwa kuripotiwa kuonya kwamba ushiriki katika sherehe ya Bwana Odinga itapelekea kufutiwa leseni zao. Taasisi za habari ambazo zimepuuza ushauri huo zimefungiwa shughuli zao,” amesema Bwana Colville.

Mapema wiki hii, kiongozi mkuu wa upinzani Kenya, Raila Odinga, alifanya sherehe yenye utatanishi ambapo alijitangaza ni “rais wa wananchi.” Serikali imefunga vituo vya televisheni ili kuzuia matangazo mubashara ya tukio hilo.

Baada ya mzozo wa uchaguzi uliogubikwa na dosari, Uhuru Kenyatta, aliapishwa kuongoza awamu ya pili kama rais mwezi Novemba. Odinga, ambaye aliyakataa matokeo ya uchaguzi, aliandaa sherehe za kuapishwa kwake akikaidi amri ya serikali, ambayo ilisema hicho kitakuwa ni kitendo cha uhaini.

Colville ameiambia VOA haamini kuwa kufungwa kwa vituo vya televisheni kumezuia ghasia ambazo zilitabiriwa kama sherehe za kujiapishwa Odinga zingefanyika kama ilivyopangwa. Anasema ni hatari sana kuhusisha matukio mawili.

Bwana Colville anasema, “ukweli ni kwamba na imekuwa ni jambo zuri kuwa sherehe, ambazo zilifanywa na chama cha Odinga zilipita kwa amani. Maelfu ya watu walihudhuria licha ya maonyo ya serikali kwamba wasifanye hivyo. Lakini, polisi walionekana kuchukua tahadhari nzuri kuepuka makabiliano wakati wa sherehe hizo.”

Wakati ambapo Colville anapongeza hali iliyojitokeza, anasema kuendelea kuvifungia vituo vya televisheni si jambo muafaka na hilo ni vyema limalizike.

XS
SM
MD
LG