Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 15:57

Serikali Kenya yaendelea kuwakamata viongozi wa NASA


Waziri wa Mambo ya Ndani Kenya Fred Matiang'i

Mbunge wa jimbo la Makadara nchini Kenya amekamatwa akiwa nyumbani kwake katika eneo la Buruburu na kupelekwa katika ofisi za makao makuu ya Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) huko Kiambu.

Mayor huyo mstaafu wa Nairobi alikuwa mstari wa mbele wakati kiongozi wa Chama cha Upinzani Nasa Raila Odinga alipokuwa akijiapisha Januari 30, 2018.

Hivi karibuni timu ya makachero iliandaliwa Makao Makuu ya DCI kuchunguza madai ya shughuli za ukiukaji sheria ambazo zilifanyika wakati wa sakata linaloendelea la kujiapisha Raila Odinga

Kile kilichokuwa kimeshuhudiwa katika viwanja vya Uhuru Park ni jaribio la kuipindua serikali ya Kenya iliyoundwa kwa mujibu wa Katiba,” amesema Waziri wa Mambo ya Ndani Matiang’i wakati akizindua kamatakamata hiyo dhidi ya Nasa.

Mara baada ya hapo ukamataji huo ulianza kutekelezwa kwa kukamatwa Mbunge wa Ruaraka TJ Kajwang na aliyejitangaza kuwa Jenerali wa Kikundi cha National Resistance, Miguna Miguna.

George Aladwa anatuhumiwa kwa kupanga shambulizi nyumbani kwa Kalonzo Musyoka na kuendesha vurugu katika eneo la Kibera.

Katika shambulizi lililotokea Januari 31, watu wenye silaha walitupa bomu la mkononi katika nyumba ya Kalonzo Karen kabla ya kurusha risasi hewani mara mbili.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Charles Owino, ambaye alifuatana na maafisa wa upelelezi kutoka ofisi za Polisi Nairobi na idara ya mabomu na usimamizi wa vitu hatarishi wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) katika eneo la tukio hilo, na kuthibitisha kuwa washambuliaji hao walitumia bomu ambalo hutumika kutishia zaidi na sio kudhuru.

Tukio hilo lilijiri masaa kadhaa baada ya Kalonzo Musyoka na viongozi wengine wa Nasa kushindwa kuhudhuria shughuli za uapishwaji katika viwanja vya Uhuru Park.

Siku ya Ijumaa Februari 2, 2018, vurugu zilitokea katika eneo la Southern Bypass na sehemu ndogo ya Kibera huko Nairobi katika kile kilichoonekana ni kupinga hatua ya polisi kumkamata Miguna Miguna.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG