Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 23:23

Serikali Kenya na upinzani Nasa zaendeleza mvutano


Raila Odinga
Raila Odinga

Mivutano nchini Kenya kati ya serikali na upinzani inaendelea kuongezeka kufuatia Raila Odinga kujiapisha Jumanne kama ‘Rais wa Wananchi.’

Siku ya Ijumaa mamlaka zimewakamata washirika wa Odinga na kuchochea maandamano katika baadhi ya sehemu za mji mkuu. Wakati huo huo serikali ikiendelea kukaidi amri ya mahakama ya kuondoa marufuku kwa vyombo vitatu huru ya habari.

Vyombo hivyo vitatu ambavyo ni vikubwa nchini humo bado havijarudi hewani kwa siku ya nne Ijumaa licha ya maamuzi ya mahakama yaliyotolewa Alhamisi kuitaka serikali ibadili uamuzi wake. Mamlaka zilikata matangazo kwa vyombo hivyo Jumanne wakati vikijitayarisha kuripoti tukio la kujiapisha kwa kiongozi wa upinzani.

Mwanaharakati wa haki za binadamu Kenya ambaye alihusika na kuwasilisha kesi mahakamani, Okiya Omtata, alijaribu kuwasilisha nyaraka za maamuzi ya mahakama kwenye ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano siku ya Ijumaa.

Omtata amezungumza na VOA na kuelezea kilichotokea baadaye.

“Mimi binafsi walinifuatilia na sikuruhusiwa kuingia. Niliambiwa kwamba walipewa maagizo kutoka juu kuwa nisiruhusiwe kuingia ndani, wala kukabidhi waraka wenye amri ya mahakama. Kwahiyo nilichofanya ni kuibandika kwenye ukuta, nakala ya amri hiyo, lakini waliamua kuichana,” Omtata amesema.

Amesema hana maamuzi isipokuwa kwenda tena mahakamani siku ya Jumatatu kulirejesha suala hilo na kuongeza kuwa hilo sana linabainisha masuala yaliyopo mbele yake, nafahamu tunakabiliana na nini siyo kushindwa kuheshimu sheria, lakini ni hatua ya makusudi ya serikali ya kukiuka haki za watu na katiba ya Kenya na kufanya mambo bila ya kujali sheria.

Mamlaka ya Mawasliano haijatoa maoni yake kuhusu marufuku hiyo. Omtata ameiambia VOA kuwa aliweza kuwasilisha baadhi ya nyaraka ambazo zilikuwa zifikishwe kwa mwanasheria mkuu, waziri wa mambo ya ndani na waziri wa habari, mawasialiano na teknolojia.

Utawala wa Jubilee unavishutumu vyombo vya habari kwa kushindwa kuheshimu ushauri waliotoa wa kutorusha tukio la kujiapishwa kwa kiongozi wa upinzani siku ya Jumanne. Katika taarifa iliyotolewa Jumatano, siku moja kabla ya mahakama kuu kutoa maamuzi yake, waziri wa mambo ya ndani, Fred Matiang’I amesema vituo hivyo vitafungwa mpaka uchunguzi unaofanyika ukamilike kuhusiana na kile alichokiita juhudi ya kuingilia kati serikali na kuchochea ghasia.

Odinga amepinga matokeo ya uchaguzi wa marudio wa Oktoba, ambao aliususia. Rais aliyepo mamlakani Uhuru Kenyatta altiangazwa mshindi.

Katika taarifa yako siku ya Alhamisi, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeelezea wasi wasi mkubwa juu ya wote kujiapishwa kwa Odinga na kile ambacho maafisa wa Marekani wamekiita “hatua ya serikali kuvifunga vituo vya habari, ni manyanyaso, na kuweka masharti kwa vyombov ya habari.”

Rais Kenyatta katika hotuba yake kwenye chuo cha serikali nchini ambayo ilirushwa moja kwa moja kwa njia ya televisheni, mwisho katika hotuba yake aliwaeleza wana habari “kwanini hamzimi vyombo vyenu, ondokeni. Kazi yenu imekwisha.”

XS
SM
MD
LG