"Serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka kurekebisha mfumo wa polisi," mashirika sita ya haki za binadamu ikiwa ni pamoja na Human Rights Watch, na Amnesty International yalisema katika taarifa siku ya Jumatano.
"Huu ndio wakati kwa nchi hiyo kushughulikia kwa umakini masuala ya kina ya ubaguzi wa rangi na ubaguzi katika utekelezaji wa sheria," alisema Ravina Sham-da-sani, msemaji wa afisi ya Umoja wa Mataifa ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu.
Wito huo ulirejelewa baada ya mauaji ya Juni 27, ya kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 17, Nahel Mer-zouk, yaliyofanywa na afisa wa polisi nje ya mjiwa Paris.
Tukio hilo lilisababisha maandamano makubwa katika takriban miji 200 kote nchini Ufaransa katika muda wa wiki moja iliyopita.
Forum