Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:06

Ulimwengu wa mitindo wapuuza ghasia Ufaransa


Wanamitindo wakionyesha mavazi ya Christian Dior huko Spain juni 16, 2022 Picha na Rodrigo Oropeza / AFP.

Mitindo ya mavazi ya Miungu ya kike ya Kigiriki ya Christian Dior, na ile ya nguva ya Iris Van Herpen pamoja na mavazi ya Schiaparelli yenye msukumo mzuri wa sanaa -- Ulimwengu wa mitindo ulipuuza ghasia nchini Ufaransa wakati wa uzinduzi wa mitindo ya mavazi ya kifahari uliofanyika Jumatatu.

Chapa ya Ufaransa ya Celine iliahirisha monyesho yake siku ya Jumapili kutokana na ghasia zilizosababishwa na kitendo cha polisi kuua kijana mwenye umri wa miaka 17 wiki iliyopita.

Lakini wakati ghasia zikisambaa katika jiji la Paris mwishoni mwa juma, shirikisho la wanamitindo lilisema halitarajii usumbufu katika wiki ya mititindo ambayo inasheherekea mavazi ya garama kubwa, yaliyoshonwa kwa kupimwa ambayo haiwezi kutenganishwa na matatizo yanayoikumba nchi katika siku za hivi karibuni.

Mbele ya watazamaji akiwemo rapa Cardi B na mhariri wa Vogue Anna Wintour, Schiaparelli alianza kwa kuonyesha mitindo ya kile kinachoitwa "mambo ya kipekee yanayopatikana ndani kabati la mwanamke".

Moja ya mitindo ilitengenezwa kwa kuchora kwa mkono mwili wa mwanamke katika mtindo wa msanii Lucian Freud na kuchapishwa kwenye soksi ya hariri.

Sweta na sketi zilitengenezwa kwa vipande vya kioo vilivyovunjwa kutokana na taswira ya mchongaji Jack Whitten, na kupongeza kwa Sarah Lucas, Joan Miro na Salvador Dali.

Jumatatu pia ilishuhudia maonyesho ya kwanza ya mbunifu wa Marekani Thom Browne na Charles de Vilmorin mwenye umri wa miaka 26, wakiwasilisha chapa yake baada ya muda mfupi kama mkurugenzi wa kisanii wa Rochas.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG