Alhamisi maelfu ya watu waliandamana kwenye kitongoji cha kifahari cha Paris cha Nanterre siku mbili baada ya afisa wa polisi kumpiga risasi Nahel M., kijana mwenye umri wa miaka 17 kwenye kizuizi cha barabarani.
Waandamanaji hao wakiongozwa na mama wa kijana huyo walisikika wakisema "Haki kwa Nahel", baadhi wakiwa na mabango yalioandikwa kwamba, "Polisi wanaua", wakati wa maandamano hayo yaliyoanza kwa amani lakini yakamalizika kwa ghasia.
Afisa wa polisi aliyempiga risasi alifunguliwa mashitaka ya mauaji na kisha kushikiliwa kwenye kizuizi cha muda.
Wakili wake Laurent Franck Lienard hata hivyo ameambia radio ya Ufaransa ya RTL kwamba afisa huyo hakuwa amevunja sheria.
Forum