Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 22:10

UN kukutana kujadili madai ya ukiukaji wa haki za binadamu Ethiopia


Mtoto akiwa juu ya mtutu wa kifaru ambacho kiliharibiwa katika mapigano ya hivi karibuni kati ya majeshi ya Ethiopia na wapiganaji wa TPLF huko Damot Kebele, mkoani wa Amhara, Ethiopia Disemba 7, 2021. REUTERS/Kumera Gemechu
Mtoto akiwa juu ya mtutu wa kifaru ambacho kiliharibiwa katika mapigano ya hivi karibuni kati ya majeshi ya Ethiopia na wapiganaji wa TPLF huko Damot Kebele, mkoani wa Amhara, Ethiopia Disemba 7, 2021. REUTERS/Kumera Gemechu

Baraza la haki za kibinadamu la Umoja wa Mataifa limeandaa kikao cha dharura kuhusu Ethiopia huku kukiwa na ripoti za ukatili mkubwa unaotokea katika eneo la Tigray.

Kikao cha leo, kinaandaliwa kufuatia ombi la Umoja wa Ulaya, kitaamua iwapo kuna haja ya kuteua timu ya kimataifa kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za kibinadamu ambayo makundi ya kutetea haki yanasema huenda yanafikia kiwango cha uhalifu wa kivita.

Mapigano ya Tigray yalianza mwezi Novemba mwaka 2020, wakati serikali ya Ethiopia ilipopeleka wanajeshi katika mkoa huo kuwazima wapiganaji wa kundi la Tigray, waliokuwa wameikamata kambi ya jeshi la serikali kuu katika eneo hilo.

Mwezi uliopita, umoja wa mataifa ulitoa ripoti ya kurasa 100 inayoelezea kwa upana ukiukaji mkubwa huko Tigray, ikiwemo mashambulizi kwenye miji, mauaji ya raia na kusambaa kwa manyanyaso ya ngono.

Wiki hii, mashirika ya kimataifa – Amnesty international, na la Human rights watch, yalielezea kwa kina ukatili mkubwa unaotokea katika sehemu hizo, ikiwemo ukamataji wa watu wengi, mateso na idadi kubwa ya watu wa Tigray waliokoseshwa makazi.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa hayana uwezo wa kuingia katika jamii nyingi ambako kumeripotiwa watu wengi wako katika hatari ya ya kukumbwa na njaa.

Umoja wa Ulaya umesema kwamba baraza la haki za kibinadamu la Umoja wa Mataifa lina jukumu la kuzuia ukiukaji wa haki za kibinadamu na kuhakikisha kwamba waathirika wanatendewa haki.

Ethiopia imefutilia mbali hatua hiyo ikisema ina ushawishi wa kisiasa.

XS
SM
MD
LG